Tuesday, 31 May 2011

FFU, WANAFUNZI WAPAMBANA

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya maandamano ya amani yaliyofanywa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tosamaganga, walioandamana kwenda katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya uongozi wa shule yao.
Tukio hilo lililowahusisha zaidi ya wanafunzi 1,000 lilitokea kati ya majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana baada ya polisi kufukuzana na wanafunzi hao kwa lengo la kuwatawanya pasipo mafanikio kutokana na wengi wao kukimbilia porini na wengine katika nyumba za wenyeji wa maeneo waliyokuwapo.
Hatua hiyo ilisababisha hali ya amani, kwa wananchi wa maeneo ya Mseke ambao kutokana na mabomu hayo walilazimika kuzihama nyumba zao na kukimbilia porini ili kuyakwepa mabomu hayo, kutoweka.
Waandishi wa habari ambao pia walikuwepo katika eneo hilo wakifanya kazi yao nao walizuiwa kuchukua habari hizo na askari polisi hadi wapate kibali kutoka polisi.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari polisi hao waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa  Polisi Wilaya ya Iringa (OCD) wakikabiliana na  wanafunzi hao.
Kabla polisi hawajafika eneo hilo wanafunzi hao kwa nyakati tofauti walisema sababu ya kufanya mgomo wa kutoingia madarasani na kutaka kuandamana unatokana na uongozi mbovu wa shule  hiyo usiozingatia haki za binadamu.
Waliyataka madai yao kuwa ni mfumo wa ufundishaji kutofuata taratibu na kanuni za ualimu, ukosefu wa vitendea kazi kama madawati na vitabu.
Mengine ni hatua ya makamu mkuu wa  shule hiyo kutumia nafasi yake kujinufaisha yeye binafsi badala ya  kusaidia kukuza kiwango cha elimu na  mengine.
Madai mengine ni kupewa chakula   kisichokuwa na ubora kama wanavyoelezwa  wazazi huku wakimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa kutolea ufafanuzi kuhusu bajeti inayotengwa kwa shule hiyo kwa ajili ya chakula.
Madai mengine ni ubadhirifu  wa mali za shule pamoja na fedha nyingine wanazochanga na matumizi mabaya ya  fedha za shule yanayofanywa na mhasibu hivyo kuutaka uongozi  wa  shule hiyo kuweka  wazi matumizi ya michango yao mbalimbali ambayo  wamekuwa  wakichangia.
“Tunataka pia kujua kuhusu ‘Fund’ ya wasomi  waliosoma hapa Tosamaganga  inatumikaje na leo tunaiomba  Wizara ya Elimu, Mkuu wa mkoa wa Iringa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi na ofisa  elimu  kufika shuleni hapa na  kuja kusikia kilio  chetu wanafunzi.”
Tanzania Daima ilipomtafuta kwa simu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, aligoma kutoa ushirikiano wowote kuhusu suala hilo kwa madai kuwa vyombo vya habari viliripoti tofauti habari ya kutekwa magari katika milima ya Kitonga.
Mkuu wa shule hiyo hakuweza kupatikana kuzungumzia madai hayo kutokana na kuhudhuria vikao mbalimbali  vilivyokuwa vikiendelea kati ya uongozi wa shule hiyo na vyombo vya dola. 

WANAMUZIKI WAREMBO WENYE MVUTO MKALI!!!!!

                                                                  RIHANA
                                                                    BEYONCE
                                                                      SHAKIRA
                                                             KATY PERRY
                                                              PUSSYCAT  DOLLS

Monday, 30 May 2011

WACHEKESHAJI WA BONGO




KIWEWE: Aliyepata umaarufu kwa kuvunja watu mbavu, 


SANAA ya vichekesho kwa hapa nchini imekuwa ikishika kasi kila kukicha kiasi cha kuweza kuliteka soko la filamu katika siku za hivi karibuni.
Kama hiyo haitoshi, sanaa hiyo imeweza kuwanufaisha wengi ikiwemo baadhi yao kuajiriwa, huku wengine wakiweza kuishi maisha mazuri.
Robert Augustino Mbumira, maarufu kama Kiwewe ni mmoja kati ya wasanii ambaye ameweza kujipatia umaarufu mkubwa kupitia sanaa hiyo ya vichekesho hapa nchini.
Katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, Kiwewe anasema anamshukuru Mungu kwa kuweza kupata ajira kupitia kipaji chake, kwani kwa sasa ni muajiriwa katika kituo cha televisheni cha EATV akifanya kazi katika kundi la Ze Comedy Show linalorusha michezo yake katika kituo hicho.
Anasema yeye pamoja na wenzake; Bambo, Mtanga, Master Face, Masawe Mtata na Dokta Rushwa walipata ajira hiyo baada ya kushinda katika shindano la Ze Comedy Search lililoandaliwa na kituo hicho, likiwa na lengo la kuwapata wasanii watakaoziba nafasi iliyoachwa wazi na wasanii wengine waliohamishia kazi zao katika televisheni ya taifa ya TBC1.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata ajira kupitia kipaji changu kwani nilisota sana katika kupata mafanikio katika tasnia hii, kweli Mungu ni mkubwa,” anasema.
Kiwewe anaongeza kuwa pamoja na ajira hiyo, pia mwajiri wao amewapa fursa ya kwenda kujiendeleza kimasomo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo.


Sunday, 29 May 2011

ManU Wameshindwa Kukifanya Kilichotakiw

Hayawi hayawi yamekuwa ndani ya Wembley, 2011. Historia ya mashindano ya mabingwa ya Ulaya leo imeweza kugeuzwa na kuandikwa kivingine kabisa. Barcelona wameweza kuchukua ubingwa huo kwa mara mbili kwenye kipindi cha miaka mitatu, kitendo amabcho hakijawahi kufanywa na timu yeyote ya Ulaya. Ulikuwa ni mchezo wa kusismumua na hauna maelezo ya kuweza kuusimulia kama ulishidwa kuweka jicho lako kwenye luninga (TV).
 
                  
Manchester United wameshindwa kufanya kilichotakiwa ambacho ni kufunga magoli na si kuzuia timu pinzani kufunga goli. Japokuwa mechi ilitawaliwa na kandanda safi kutoka kwenye timu zote mbili lakini mshindi alikuwa katoka timu kwenye timu moja ambaye ni Lione Messi. Messi aliyeiongezea matumaini yake kushinda mechi hiyo baada ya kuachia mkwaju mkali kutoka nje ya eneo la hatari kwenye lango la Manchester United na kuiandikia timu yake bao la pili.                                             


                           
Kwa hakika kikosi hiki cha Barcelona kinastahili ubingwa kwa mchezo na ufundi waliouonyesha uwanjani.  Ila swali linabaki kwa kocha wao kijana anyechipukia kwenye hii taaluma ya kufundisha  kabumbu kama atabaki na timu hii msimu ujao. Minong’ono iliyopo ni kuwa hii itakuwa mechi yake ya mwisho kwa Barcelona basi tusubiri kwa hilo. Mlango wa timu ya Chelsea bado uko wazi waungwana lakini swali ni kwanini anataka kuondoka kwenye timu kama hiyo ina kila kitu ambacho watu wengi wanafikiria kuwa navyo?
                       

DILLY KALUNGA MREMBO WETU WA MAN U {GOD BLESS MAN U}




ETI AMINI NA LINA WAMEMWAGANA!!!!!


Uhusiano wa kimalavidavi uliovuma sana kwenye vyombo vya habari wa wasanii toka THT,Linah na Amini umefikia kigoma mwisho wa reli baada ya kila mmoja kufunguka kuwa wamemwagana...!

AMINI MWINYIMKUU na LINAH SANGA WOTE NI BONGO FLAVA ARTIST, WALIFUNGUKA NA KUSEMA,

Linah alifunguka “Tulikaa tukakubaliana na kila mmoja akaridhia kuwa iwe mwisho wa uhusiano wetu hivyo sababu siwezi kuweka wazi ila mashabiki wangu wajue tumeachana,”...Huku Amini nae alisema....“Dah! bwana ndiyo hivyo kila mtu kwa sasa yupo kivyake ila uelewe sipendi kuzungumzia uhusiano wetu sababu haunisaidii chochote katika muziki wangu.” Inasemekana kuwa wimbo aliouimba Linah wa Bora Nikimbie ulikua ni kutoka moyoni coz inadaiwana Amini alikuwa na tabia ya kumpa kipigo Linah mara kwa mara kitendo ambacho alikuwa anakivumilia na kufikia hatua ya kumwagana!

" Kwa kweli walipotoa tu nyimbo zao zijulikanazo kama Bora nikimbie wa Linah na Ndiyo unikimbie wa Amini, watu walishajua kabisa kwamba hawa wasanii wamemwagana na sasa kila mmoja anatafuta jinsi ya kutoa machungu yake baada ya kuachana".




. UOTE OF THE DAY….!!!



It’s better to hang out with people better than you. Pick out associates whose behavior is better than yours and you’ll drift in that direction. Warren Buffett.

Friday, 27 May 2011

TUBORESHE VAZI LA AFRICA.







NI WAZI KUWA MOJA ALAMA INAYOMTAMBULISHA NA KUMTOFAUTISHA MWANADAMU MMOJA NA MWINGINE,AMA TAIFA MOJA NA LINGINE NI UTAMADUNI,TUBORESHE UTAMADUNI KWA AJILI TAIFA AU MATAIFA,VIZAZI VINAVYOKUA NA VIJAVYO..MMEPENDEZA WADADA.

Thursday, 26 May 2011

DOKII NA MAKALIO YA KICHINA.

MWANADADA Ummy Wenceslaus, aliye maarufu kwa jina la Dokii ambaye ni muigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza, ameibuka kujibu tuhuma za baadhi ya watu wanaodai makalio yanayoonekana kwenye filamu yake ya ‘Scandal’ ni ya Kichina.
Akizungumza na Sayari, Dokii alisema watu hao wamekosa la kuongea kwani makalio wanayoyaona ni ya kwake ya kuzaliwa nayo, na kuongeza kuwa anamshukuru mama yake kwa kumzaa na maumbile hayo ambayo yanatatanisha watu hadi kuyaita ya Kichina.
 “Nataka waelewe kuwa yale ni maumbile aliyonijalia Mwenyezi Mungu, na wala sina mpango wa kuingia kwa Wachina kumkosoa Muumba,” alisema mwanadada huyo ambaye ni mlokole.
Akiongelea kuhusu sababu ya kuigiza filamu hiyo inayoonyesha bubu akiwa anafanya shughuli za uchangudoa, Dokii anasema ameamua kuja kitofauti, kwani watu wengi amewaona wakipenda kuigiza ulemavu wa kutembea na upofu, huku wakisahau kama kuna wale wasioweza kuongea.
Aidha, alisema ujumbe wake aliokusudia kuufikisha kwa jamii, ni watu kumuogopa Mungu, kwani pamoja na ulemavu aliokuwa nao Surprise wa kwenye ‘Scandal’, lakini watu walikuwa wakimfanyia sivyo ikiwa ni pamoja na marafiki zake.

Wednesday, 25 May 2011

MMMMHHHHHH!!!!!! NYIE MAPACHA AU? KAZI KWA WADAU?

                                  SELE MBONDA  FROM DALLAS, TEXAS(USA)






                                         SIDE MBEGU FROM STOCKHOLM, SWEDEN








Mzee sele na side mbona kama mnafanana  kazi kwa wadau wanaonaje ila MANSHA ALLAH MMEPENDEZA NA ALLAH MA'AK.

Tuesday, 24 May 2011

DUNIANI WAWILI WAWILI.










Aliyeumba mwanzo aliumba mtu mume na mtu mke, kwahiyo  mtu atamwacha babaye na mamaye na kuambatana na mumewe au mkewe  na kua kitu kimoja . MMEPENDEZA SANA , MBARIKIWE.