Thursday, 21 July 2011

BABY J AJITOSA BIFU LA AT NA Off SIDE TRICK!!!!!!!!!





 BIFU lisilojulikana mwisho wake lini baina ya wasanii wa muziki wa bongo fleva ambao wana asili ya visiwani Zanzibar, linazidi kuchukua sura mpya.
Katika bifu hilo, walianza AT na kundi lake la zamani la Off Side Trick, na sasa mwanadada Baby J naye ameingia.
AT na Off Side Trick wamekuwa wakitupiana vijembe kupitia nyimbo zao, bila kujulikana hasa chanzo cha ugomvi wao ni nini.
Lakini wakati mashabiki na wadau wa muziki wakishindwa kubaini chanzo baada ya Off Side Trick kutoka na wimbo wao ‘Kidudu Mtu’ na AT akawajibu na ‘Vifuu Tundu’, Baby J ametoka na ‘Domo Kaya’ akimshirikisha Gelly wa Rhymes.
Wimbo huo wa Baby J unadaiwa kuwa ni kijembe kwa AT.


NGWAIR ANAKUPA KITU B.B.M!!!!!!!!!


MKALI wa mitindo huru (free style) nchini, Albert Mangwea ‘Ngwair’ muda si mrefu ataachia ngoma mpya inayokwendwa kwa jina la B.B.M.
Black Beauty Model ndiyo kirefu cha BBM na kibao hicho kimerekodiwa katika studio za Bongo Records chini ya mtayarisha P-Funk Majani.
Ngwair amesema kama kawaida wimbo huo utakuwa mkali kama ilivyo nyimbo zake zilizowahi kutoka nyuma.
Mkali huyo toka Chamber Squad amewahi kutamba na singo kama ‘Gheto Langu’, ‘Hostel’ na nyinginezo.

DUDU BAYA AGEUKIA FILAMU!!!!!!!!!!!

MKALI wa bongo fleva nchini, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ amegeukia filamu ambapo tayari ameshacheza mbili mpaka sasa.
Kugeukia kwake katika filamu kunaongeza idadi ya nyota wa muziki huo waliojaribu katika upande wa pili wa sanaa, wakiwemo Q Chillah, Ali Kiba, Mr. Blue na wengineo.
Kazi ya kwanza ya Dudu inakwenda kwa jina la ‘The Musk’ huku pia akiwa mbioni kupakua movie yake ya pili iitwayo ‘The Leopard Ghost’ ambayo ndani yake atakuwemo msanii mwenzake, Hemed Suleiman.
Aidha, Dudu amebainisha kwamba ndani ya ‘The Leopard Ghost’ amecheza kama rafiki wa Hemed, pia mwanamuziki

Saturday, 16 July 2011

BWANA MISOSI KUWASHA MOTO NDANI YA BILICANAS!!!!!!!!!!!!




UKUMBI wa kimataifa wa Club Bilicanas, Jumapili unatarajiwa kupambwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa msanii mahiri wa muziki wa bongo fleva, Joseph Rushahu maarufu kama Bwana Misosi.
Mkali huyo ambaye amekuwa akiibuka na kutoweka katika tasnia hiyo, atatumbuiza ukumbini hapo kupitia usiku maalumu wa Bongo Starz Nite ambao kwa Jumapili ijayo umebatizwa jina la ‘Usiku wa Misosi na Bwana Misosi’.
Bwana misosi ni mmoja kati ya wasanii waliojipatia umaarufu mkubwa hapa nchini na nchi jirani, hiyo inatokana na umahiri mkubwa katika utayarishaji wa kazi zake ambazo zimekuwa zikiwashika mashabiki.
Tayari Bwana Misosi amefanikiwa kuachia albamu tatu mpaka sasa, ambazo ni ‘Nitoke Vipi’ (2004),  ‘Kazi  Yangu’ (2006)  na ‘Pilato na Game’ (2011), huku singo ya ‘Kipusa’ aliyomshirikisha Prof. Jay ndiyo ilikuwa ya kwanza kwake, ambayo kwa kiasi chake iliweza kumtambulisha.
Singo ya ‘Nitoke Vipi’, ndiyo iliyomtambulisha katika medani ya muziki huo alipoanza rasmi mwaka 2005 ambapo ndani yake anawauliza mashabiki atoke vipi katika muziki huo. Kwa kifupi wimbo huo ulifanikiwa kukamata sana kuanzia kwenye redio, televisheni na hata kumbi za starehe.
Hakuishia hapo, kwani alikuja na singo ya ‘Mabinti wa Kitanga’ ambayo ndani yake ilikuwa ikielezea sifa za mabinti wa mkoani Tanga, ikiwamo kujua kujipamba, mapozi na mambo mengine.
Ukali wake unatokana na kuimba nyimbo zenye ujumbe mahususi kwa jamii, hivyo kumtofautisha na wasanii wengine; mfano katika singo ya ‘Pilato na Game’ aliomshirikisha Fid Q anazungumzia matatizo yanayoikumba sanaa ya muziki na wasanii kwa ujumla.
Pia mustakabali mzima wa muziki akizungumzia kuhusu wingi wa watayarishaji wa muziki kila mahali tofauti na zamani, huku akilinganisha mambo yanayotokea sasa katika muziki ni sawa na kilio ambacho anakileta kwa mashabiki ili wajue hasa nini kinachosumbua.
Katika moja ya mashairi yake kwenye wimbo huo Misosi anaimba: “…Maprodyuza kibao, sina imani na mwongozaji wa mchezo mpaka fulani ndo promo usogezwe, …refa anashabikia timu pinzani offside center hivi kweli nitawini….namuamini Mungu namba moja kitu gani, …nimejipanga simjui rafiki, adui, kasuku, kinyonga, simba, swala, mbogo na chui, si ufisadi sanaa ingekuwa mbali nafasi nikipewa nachekea nyavu kweli… ”.
Anaendelea: “Kwa mfano enzi za kifalme pilato watoza ushuru South Afrika enzi zile za Mkaburu, Tanganyika na mapinduzi ya uhuru, same time kumuweka wangu …wala sikufuru makamisaa wapo, refa anawaburuza, muuaji wa vipaji tapeli wanamtukuza, mashabiki nanyi mmelishwa limbwata kukubali tembo mtamu kuliko nyama ya bata, upande wao ni furaha….iwe ni mamba au kenge wanaongoza tu msafara….imani matendo ni tofauti na kuokoka…”.
Pia amewahi kutoka na singo kama; ‘Heshima’ aliyomshirikisha Red Sun kutoka Kenya, ‘Huwezi jua’ aliyomshirikisha Jua Cali kutoka Kenya, ‘Mungu yuko bize’ aliomshirikisha Chegge, ‘Nimesomeka’ aliomshirikisha Nikki Mbishi na nyingine kibao ambazo zote zimekuwa zikifanya vema.
Akiwa mmoja wa wasanii wenye asili ya Mkoa wa Kigoma, aliyekulia mjini Tanga ambao wanawakilisha vema katika medani ya muziki, Misosi amekuwa akija na kupotea katika tasnia hiyo, huku mwenyewe akidai kuwa ni kutokana na kutingwa na shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwemo masomo.
 “Ukimya wangu ulikuwa unamaanisha, kwani nilikuwa darasani kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, sasa hivi nimerejea rasmi kwenye game,” alisema Misosi ambaye alikuwa akisomea masuala ya teknolojia ya habari (IT).
Anaongeza kuwa, kwa sasa amerudi kwa nguvu zote huku akiwaomba mashabiki wa muziki huo nchini kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake kama walivyokuwa wakifanya tangu aibuke.
“Mambo mazuri zaidi na zaidi yanakuja, mashabiki watarajie kazi nzuri kutoka kwangu, pia watarajie kuniona kwenye majukwaa ya muziki katika sehemu tofauti nchini na hata nje ikiwezekana,” alisema.
Mkali huyo ameweza kuwa mmoja kati ya wasanii bora wa muziki huo kiasi cha kushinda tuzo za muziki za Kili mwaka 2009/2010 kama mwimbaji bora wa reggae kupitia singo yake ya ‘Mungu yupo bize’.
Akizungumzia hali ya muziki nchini, Bwana Misosi anasema imekuwa ikikua kila kukicha, na hivyo kuwepo kwa ushindani mkubwa baina ya wasanii na wasanii na bila kuumiza kichwa msanii anaweza kujikuta akibaki kuwa msindikizaji kama si kushindwa kufanya alichokusudia.
Hata hivyo, Bwana Misosi anasema ni wasanii wachache ambao wameweza kudumu katika medani hiyo hiyo kwa muda mrefu, na hiyo inatokana na umakini walionao na kutambua nini wanachokifanya.
 “Wengine wanaingia kwa kufuata mkumbo, kupata umaarufu n.k, lakini mambo ya ulimbukeni, utovu wa nidhamu na kuvimba kichwa ni baadhi ya mambo yanayochangia kuwamaliza wasanii wengi katika muziki,” anasema
Akiwa na matarajio ya kufika mbali zaidi katika medani hiyo, mkali huyo pia anawaasa wasanii wenzake kujiheshimu sambamba na kutunga nyimbo zenye ujumbe muhimu kwa jamii badala ya kuimba sana nyimbo za mapenzi

MUSA KITALE ANATARAJIA KUACHIA FILAMU "MORE THAN LION"

MSANII wa vichekesho na maigizo, Musa Kitale, aliye maarufu kwa jina la Kitale, hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘More than a Lion’ ambapo ndani yake amemshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja wa kundi la Tip Top Connection.
Kitale alisema katika filamu hiyo ambayo amecheza kama mhusika mkuu, anaonekana kuwa mkali sana kwa wadogo zake, mpaka anajikuta anaharibu.
Katika filamu hiyo ambayo alisema ipo katika hatua za mwisho kuihariri, amewashirikisha pia wasanii wengine aliocheza nao katika tamthilia ya Jumbo la Dhahabu kama vile Mzee Kaangaa, Kisosi na Aunt Kame.
Hata hivyo Sayari ilipomdodosa ili kujua kama alishawahi kutumia mihadarati kidogo kutokana na michezo mingi kupenda kuigiza kama teja, Kitale alisema hajawahi na wala hatumii kilevi cha aina yoyote.

Friday, 15 July 2011

" UJIO" AMEAMUA KWENDA DARASANI (UDSM) KUSOMEA FANI YA SANAA

MSANII wa maigizo, Netho Nazareti  ‘Ujio’, ameamua kwenda darasani ambapo sasa hivi yupo mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea fani ya sanaa.
 Ujio ambaye jina lake lilitamba katika kundi la Kaole, akiigiza kama zezeta, alisema ameamua kwenda darasani baada ya kuona kuwa kufanya fani ya sanaa bila elimu ni kazi bure.
Ujio anasema baada ya kwenda shule ameweza kupata uelewa mpana kuhusu fani nzima ya sanaa na kuongeza kuwa, kwa sasa uigizaji wa wasanii wengi hapa nchini ni wa ku – ‘copy’ na ku – ‘paste’.
 “Kwa mfano katika suala la mavazi, mtu anachoigiza ni tofauti na kile anachokivaa, lakini huku chuo tunafundishwa jinsi gani unatakiwa uende sambamba na vitu hivyo,” anasema.
Matarajio yake baada ya kumaliza chuo, anasema ni kufungua studio yake ya kutengeneza filamu, ambayo anadai kutokana na kupikwa chuoni kuhusiana na suala zima la utengezaji wa filamu, itakuwa tishio kwa studio zingine.

JE MPENZI ANAPOKATAA USIENDELEE KAZI YAKO INAKUWAJE?

MSANII wa maigizo na filamu, Zuwena Saidi ‘Anita’, amedai ukimya wake kwa muda mrefu katika game la filamu ulitokana na mchumba wake kumkataza kushiriki katika tasnia hiyo.
Anita ambaye alikuwa kivutio sana katika filamu ya ‘Mahabati’ iliyotengenezwa na Mussa Banzi,  kwa muda wote ambao alikuwa haonekani katika filamu, alikuwa akijaribu kumwelewesha mpenzi wake kuhusu tasnia ya filamu na jinsi ilivyomuingia kwenye damu.
Mbali na kusimama katika filamu, pia alilazimika kujitoa katika tamthilia ya ‘Cinderela’ inayorushwa na kituo cha Star Tv ili amridhishe mwenza wake huyo.
Hata hivyo, anasema kwa sasa anashukuru kuwa mpenzi wake huyo amemuelewa na kubainisha kuwa endapo kuna mtu yeyote atamuhitaji kucheza filamu yupo tayari.
Mbali na kuwika katika filamu, pia Anita alikuja juu baada ya kuonekana katika wimbo wa Matonya unaokwenda kwa jina la ‘Anita’, na ndiko huko jina hilo lilipomganda hadi leo

Friday, 8 July 2011

CONFIRMATION SERVICE FOR BLANDINA ANDREW AT ST ANNES SWAHILI SERVICE

                                                          BLANDINA ANDREW













The spiritof wisdom and understanding,The spiritof counsel and might,The spirit of knowledge and the fear of the lord,The spirit of joy in your presence, Both now and forever. AMEN

Thursday, 7 July 2011

H BABA ATHIBITISHA UHUSIANO WAKE NA FLORA MVUNGI!!!!!!!!!!

                                                            FLORA MVUNGI
                                                                   H BABA                                                                                  

MSANII wa muziki wa bongo-bolingo na muigizaji wa filamu, Khamis Ramadhani ‘H Baba’, ameamua kuweka mambo hadharani kuwa, kwa sasa mchumba wake ni muigizaji Flora Mvungi.
Akizungumza katika jukwaa la sanaa linalofanyika kila Jumatatu katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ilala Dar es Salaam, alisema haoni haja ya kuficha uhusiano huo kwa kuwa yeye si mapepe.
“Jamani najua mshasikia tetesi kwamba mimi najiachia na mrembo huyu, sasa leo nawathibitishia kuwa ni kweli kabisa, na ninampenda sana, japokuwa ya baadaye anayajua Mungu,” alisema.
Hata hivyo, aliuhakikishia umati huo kwamba Flora ndio msichana wake wa pili kutembea naye baada ya kuachana na Irene Uwoya, na kuwaponda baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakificha mahusiano yao.
“Hawa hawana msimamo katika mapenzi, na kuwa wazi wanaona wanaweza kutoswa na wanawake wengine pindi watakapowatokea,” alisema.
Kuhusu kuachana na Uwoya, alisema kulichangiwa na kuchafuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari wakati wa mahusiano yao na kuongeza kuwa, mama yake ndiealishinikiza kuachana na mrembo huyo baada ya kutopendezewa na tabia zake. 

WASHIRIKI WA REDD'S MISS KINONDONI WAKIWA KWENYE MAZOEZI!!!!!!









WASANII WANAPENDA KUANDIKWA MAGAZETINI?

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halijawahi kupelekewa malalamiko yoyote na baadhi ya wasanii kuandikwa vibaya na magazeti mbalimbali hapa nchini, hasa yale ya udaku.
Hayo yalisemwa na Afisa Habari wa baraza hilo bi Agnes kimwaga.
Alisema hawajawahi kupelekewa malalamiko na msanii yoyote kuwa amechafuliwa na gazeti au chombo chochote cha habari, hivyo kwa upande wake anaona kama huenda wasanii hao wanapenda kuandikwa.
Kuhusu taratibu za kuwasidia wasanii mbalimbali hapa nchini, Kimwaga alisema wamekuwa wakikutana nao kila Jumatatu ili kujua changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika kazi zao na kuzipeleka katika ngazi za juu, lengo likiwa katika kuboresha kazi zao, ambapo alidai kadiri siku zinavyozidi kwenda idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka.

Wednesday, 6 July 2011

MONACO ROYAL WEDDING!!!!!!!!!!!!!

                                                                    princess charlene of monaco

                                                             prince albert 11 and princess charlene of monaco








                                                                     karl lagerfeld

                                             queen silivia and king carl gustaf xvi
                                               naomi campbell and vladislav doronin
                                                              giorgio armani



Tuesday, 5 July 2011

HATIMAYE DAR PLUS KUTUA BONGO!!!!!!!!!!!!

DAR PLUS ni Jarida jipya ambalo liko njiani kuingia mtaani mda si mrefu. Jarida hili ni maalum kwa ajili kutoa matangazo na kutangaza biashara ya aina yoyote ikiwepo mitindo, burudani, michezo na matukio mbali mbali kutoka kwenye pande zote za dunia. Vile vile  litakuwa likiwaletea habari motomoto pamoja mahojiano ya watu mashuhuri wanaotoa mchango katika jamii yetu. 


Kwa maelezo zaidi na gharama za matangazo piga simu namba +255 657 975 747  au +255 655 454 162

Asanteni
DAR PLUS GROUP