Sunday, 18 September 2011

HAPPY BIRTHDAY CHARLES KISWANTA!!!!!!!!!!!!

IT'S TIME YOUR BIRTHDAY.........TIME FOR A SLAP-UP MEAL,DRINK... DRINK......DRINK,
HOPE YOU HAVE GREAT FUN,GOOD LUCK IN THE COMING YEAR.



                         GOD BLESS U CHARLES KISWANTA

Friday, 16 September 2011

AUNT EZEKIEL, JB, RICH, NDANI YA ISIDINGO!!!!!!!!!!!!!!!


                                                                   



KATIKA kuonesha kuwa kazi za wasanii wa filamu nchini zinakubalika hata nje ya nchi, wasanii Jacob Stephen ‘JB’, Single Mtambalike ‘Rich’ na Aunt Ezekiel, wametakiwa kwenda kuigiza katika tamthilia ya Isidingo nchini Afrika Kusini inayorushwa nchini na kituo cha televisheni cha ITV.
Hayo yalibainishwa wiki hii na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la Wasanii, Michael Sangu, wakati wa mahojiano katika kipindi cha TAGz kinachooneshwa katika kituo cha televisheni cha DTV.
Sangu alisema tayari wameshapata barua ya kuombwa kwa wasanii hao kutoka katika kampuni inayotengeza tamthilia hiyo iliyopo Afrika Kusini, na sasa wako katika hatua za kuwakutanisha ili waweze kuingia mikataba.
Aidha, mjumbe huyo aliongeza kuwa, hata waliotengeza filamu ya Neria nao wameshaonesha nia hiyo ya kuwataka wasanii hao wanaotamba katika tasnia ya filamu nchini.

LUCY KOMBA ASHUKURU!!!!!!!!!!!!!!!!!!

.

MWIGIZAJI Lucy Komba, amesema anashukuru kuungwa mkono na wafanyakazi wenzake katika kazi zake za filamu. Mwanadada huyo ambaye ni karani katika Mahakama Kuu, alisema kazi yake hiyo haimzuii kufanya kazi zake za filamu, kwani zaidi anachoona yeye ni kuzidi kupata ‘support’ kutoka kwa bosi na wafanyakazi wenzake jambo linalompa faraja.
Pia ametanabaisha kuwa, wakati wa likizo hujichimbia zaidi na kufanya kazi hizo za filamu, fani ambayo anadai alianza kuizimikia tangu alipokuwa na umri mdogo.

HEMED NA MLELA KUMALIZA BIFU.....KUAMUA KUCHEZA FILAMU "RED MZULA"



KATIKA kuonesha kuwa, Watanzania wanapenda amani, wadau wa filamu nchini wamefurahishwa na taarifa kwamba wasanii wawili wanaotesa katika anga za filamu, Yusuph Mlela na Hemed Suleiman wamemaliza bifu lao la muda mrefu na kuamua kucheza tena filamu moja inayoitwa ‘Red Mzula’ inayotarajiwa kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa., baadhi ya mashabiki hao, walisema hii ndiyo desturi ya Watanzania na si kama vijana hao walivyokuwa awali wakirushiana madongo katika vyombo vya habari, na hata kufikia hatua ya kuzichapa kutokana na sababu ambazo hazikufahamika, huku kila mmoja akijiona yuko juu zaidi ya mwenzie.
“Kwa kweli tunasubiri hiyo filamu kwa hamu ili tujionee wawili hawa jinsi ambavyo wamejiachia, kwani bifu si ishu na isitoshe inawashushia thamani waliyo nayo wasanii hao, napongeza sana hatua waliyofikia ili kuweza kuendeleza tasnia hii ya filamu,” 

JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MKEWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, imemhukumu Haruna Ndayage (54), mkazi wa mtaa wa Kashaulili, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuingilia mkewe kinyume na maumbile.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Desdel Magezi, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.
Alisema shahidi wa tano ambaye ni daktari aliithibitishia mahakama kuwa mlalamikaji baada ya kufanyiwa uchunguzi iligundulika kuwa aliingiliwa kinyume na maumbile yake.
Aidha, alisema ushahidi uliotolewa na watoto wao ulionyesha kuwa Haruna alimfayia kitendo hicho mkewe, kwani watoto wote walimtaja baba yao ndiye mhusika wa kitendo hicho.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu, kwani wakati akifanya kosa hilo hakuwa na akili timamu.
Alidai kwa miaka 24 waliyoishi na mkewe hakuwa na ugomvi wowote naye isipokuwa miezi sita kabla ya tukio hili waalikuwa na ugomvi ugomvi ambao hakuweza kuueleza mahakamani hapo.
Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Finias Mjula, alipinga utetezi huo na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili awe mfano kwa watu wengine wenye tabia ya kuwadhalilisha wake zao.
Awali katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Oktoba 28, mwaka jana, majira ya saa 12 alfajiri, mshtakiwa alimwingilia kinyume cha maumbile mkewe.