Mkuu wa Polisi eneo la Pwani ya Kenya Bwana Aggry Adoli amethibitisha tukio hilo akisema kuwa wanakijiji waliwaona watu walioshukiwa kuwa wanachama wa MRC wakiingia msituni na kuwafuata na kisha kuwaua baadhi ya watu waliokuwa kwenye kundi hilo.
Duru zinasema kuwa watu hao walikuwa miongoni mwa watu walioshukiwa kuwa majambazi.
Walikamatwa na silaha za kijadi kama vile panga na visu. Polisi wanasema kuwa mmoja wao alikuwa mganga wa kienyeji
Eneo la Pwani mwa Kenya limekuwa na migogoro ya kila aina kuanzia kwa uhasama kati ya jamii hasimu zinazoishi pembezoni mwa mkoa huo.
Polisi wamekua wakilaumiwa kwa kukosa kudhibiti ulinzi mkoani humo hasa wakati huu wa heka heka za maandalIzi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi mwaka ujao.
Hata hivyo bwana Adoli anasema kuwa utovu wa usalama sio kosa la polisi bali ni kutokana na matatizo yanayokumba jamii za eneo hilo.
chanzo:bbc

No comments:
Post a Comment