Tuesday, 31 July 2012

ULIMBOKA 'ATIKISA' BUNGE

SAKATA la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, limeibuka upya bungeni baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuitaka Serikali itoe majibu ya kina kuhusu watendaji wake kutajwa kuhusikana na tukio hilo.


Kambi hiyo pia imeitaka Serikali ieleze sababu za watendaji hao kutokamatwa hadu sasa na kuhojiwa na vyombo vya dola, wakati kuna taarifa kuwa wanafahamika.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu  hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, katia mwaka wa fedha wa 2012/13,  Conchesta Rwamlaza alisema, haiwezekani Serikali kuendelea kukaa kimya wakati watendaji wake wanatajwa kuhusika katika tukio hilo.

Rwamlaza alikuwa akizungumza kwa niaba ya msemaji wa kambi hiyo, Dk Antony Mbassa, ambaye alitaka uchunguzi huru ufanyike kuhusu kubaini ukweli.

"Aidha kwa kuwa Serikali imetuhumiwa kuhusika, kambi rasmi ya upinzani, inasisitiza haja ya kuundwa kwa tume huru ili kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo. Taarifa iliyotolewa na polisi kuhusu kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa raia wa Kenya, haipaswi kutumika kama kisingizio cha kuzuia mjadala na haiwezi kuwa kizuizi cha uchunguzi huru kuendelea kufanyika," alisema Rwamlaza.


Katika hatua nyingine, Rwamlaza alilaani kitendo cha Bunge kuzuia mjadala wa kibunge kuhusu tukio la kutekwa kwa D Ulimboka, akisema hata kama limefanya hivyo kwa kutumia kanuni, siyo sahihi.
Kambi hiyo ilisema tukio la Ulimboka linapaswa kufikishwa  bungeni ili lijadiliwe na kwamba Bunge halipaswi kuwekewa vikwazo vya kikanuni katika kujadili matatizo ya wananchi.

Kambi hiyo ilienda mbali zaidi na kukituhumu kiti cha Spika kwamba kinachangia mgogoro wa madaktari unaoendelea nchini, kwa kuzuia mijadala iliyoombwa na wabunge kuhusu suala hilo ambalo hatima yake ni kuwasitishie leseni madaktari 319.

"Kama Kiti kingetoa fursa kwa Bunge kujadili na mwisho kutoa ushauri au maazimio yake kwa Serikali, jambo ambalo ndio wajibu wetu kwa mujibu wa katiba ibara ya 63, mgogoro huo usingeendelea kudumu kwa muda mrefu na kuleta athari zaidi katika sekta ya afya," alisema.

Rwamlaza alisema "kanuni zinazolizuia Bunge kujadili masuala ya wananchi kwa kisingizio kuwa masuala hayo yako mahakamani, zinadumaza demokrasia ya nchi yetu, zinalipora Bunge haki yake ya kikatiba ya kuisimamia Serikali na zinawakandamiza wananchi wanyonge ambao hawana pa kusemea isipokuwa kupitia Bunge lao."

Alielezea kushangawa kwake na Bunge kuzuiwa kujadili suala hilo kwa maelezo kuwa liko mahakamani, wakati Rais Jakaya Kikwete alilizungumzia katika hotuba yake kwa taifa, ya Julai mosi mwaka huu. na kulitolea maagizo mbalimbali.

"Kambi ya upinzani inataka kujua kama kitendo cha Baraza la Madaktari Tanganyika kusitisha usajili kwa madaktari 319 kuanzia Julai 11 mwaka huu ni sahihi wakati madaktari hao walikuwa wameshtakiwa mahakamani kwa shauri hilo," alisema.

Alisema kutokana na upungufu huo, kambi ya upinzani inapendekeza Bunge liazimie kuwa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma kwa Jamii, iliyoshughulikia mgogoro kati ya Serikali na Madaktari, iwasilishwe bungeni taarifa ya jambo hilo  na kujadiliwa kabla ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.

"Hatua hiyo italiwezesha pia Bunge kupitisha maazimio ya kuishauri na kuisimamia Serikali kuhusu namna ya kushughulikia vyanzo vya migogoro katika sekta ya afya," alisema na kuongeza;

'Kitendo cha kuwadharau, kuwadanganya madaktari na hatimaye kuwafutia leseni madaktari 319 wa mafunzo kwa vitendo, ni kujikanganya kwa Serikal. Ni uamuzi unaoonekanaa umechukuliwa kwa kukomoa na kwa ubabe bila kujali maslahi ya taifa na afya za wananchi. 
Mgogoro mzima unaashiria uwezo finyu wa Serikali katika kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano na ukosefu wa dhima ya kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM," alisema.

Alisema kambi ya upinzania, inasikitishwa na kitendo cha Serikali kushindwa kutumia busara katika kutafuta ufumbuzi wa madai ya vitendea kazi na stahili za madaktari, jambo ambalo lilisababisha migomo ya madaktari nchini.

Hata hivyo akiwasilisha hotuba yake ya wizara bungeni jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alisema Serikali imesikitishwa na tukio la kutekwa, kuteswa na kutelekezwa msituni kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk  Steven Ulimboka.

"Serikali inatoa pole kwa ndugu Ulimboka na inamtakia kupona haraka ili aunganike na familia yake," alisema Dk Mwinyi.
Mapema waziri huyo alieleza historia ya mgogoro wa madaktari na Serikali akifafanua kuwa kwa upande wake, Serikali ilijitahidi kadri ilivyoweza  kuhakikisha kuwa unamalizika. Mwisho
chanzo:http://www.mwananchi.co.tz

ALIYETAKA KUMUUA MANDELA JELA MAISHA.


MHUSIKA mkuu wa mpango wa kumuua Nelson Mandela, wiki iliyopita katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo alipatikana na hatia ya uhaini kwenye kesi moja iliyodumu kwa takriban miaka 10 na atahukumiwa jela maisha.
Mike du Toit alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu na kiongozi wa kundi la kibaguzi la Jeshi la Kaburu la Chama cha Boeremeg, baada ya kupatikana na hatia na mahakama kusema atahukumiwa siku zijazo kuhusiana na jaribio lililoshindwa la kumpindua Mandela mwaka 2002 nchini Afrika Kusini, wanasheria akiwemo Steve Mhokholo, wamefunguka na kusema hukumu yake itakuwa kifungo cha maisha jela.
Mashahidi waliieleza mahakama kuwa du Toit na wenzake walipanga kumuua Mandela ambaye mwaka 1994 alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini pia walikusudia kuwapiga risasi weupe wenzao ambao wangepinga mtazamo wao wa kuwa taifa kamili la kibaguzi la Makaburu.
Du Toit alitaka kukiondoa madarakani kwa nia ya mapinduzi chama tawala cha African National Congress (ANC) na mahakama kuu nchini humo imesema atahukumiwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Ilidaiwa kuwa du Toit angefanikiwa kumpindua Mandela angewafukuza Waafrika wapatao milioni 40 kwa kuwalazimisha kwenda kuishi Zimbabwe tena basi wakiwa na vifurushi tu vya chakula na Wahindi wangepakiwa katika boti na kupelekwa kwao India.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

HII NI ALAMA YA..................?


WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA.



NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na walimu katika ngazi ya usuluhishi.Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa walimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

Waandishi wetu katika sehemu mbalimbali nchini pia waliripoti kwamba katika baadhi ya shule, wanafunzi waliruhusiwa kurejea nyumbani mapema kwa maelezo kwamba hakukuwa na masomo.Hali hiyo ilizua kizaazaa kwani katika baadhi ya mikoa wanafunzi walicharuka na kuitisha maandamano hadi katika ofisi za maofisa elimu wa wilaya, wakitaka Serikali iingilie kati mgomo huo ili waendelee kusoma.

Kadhalika, baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali walinukuliwa wakitoa matamko ya kuwasihi au kuwaamuru walimu warejee madarasani, kauli ambazo hata hivyo, hazikubadili uamuzi wa walimu hao.

Wanafunzi waandamana
Maandamano ya wanafunzi yaliripotiwa katika Mji wa Tunduma, Mbeya ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwadhibiti wanafunzi.
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/25164-mtikisiko.html

MAMBO YA WAGANGA WA KIENYEJI:Voodoo Man Slaps Baldy

WASIOOANA WAPIGWA MAWE HADI KUFA MALI.

Mwanamume na mwanamke huyo walizikwa mpaka kwenye shingo na kupigwa mawe hadi kufa.

Kaskazini mwa Mali nusu yake inaendeshwa na waasi wa Tuareg na wapiganaji wa Kiislam baada ya mapinduzi katika mji mkuu wa Mali.
Aguelhok katika eneo la Kidal alikuwa ni wa kwanza kukamatwa na waasi wa Tuareg .
Waislamu katika eneo la Aguelhok waliwapiga mawe mpaka kufa watu hao mbele ya watu 200 maafisa wamesema.
"Nilikuwepo. Wapiganaji hao wa Kiislamuwaliwachukua watu hao katikati ya Aguelhok. Watu hao waliwekwa kwenye mashimo mawili na wakapigwa mawe mpaka wakafa." Afisa wa serikali eneo hilo alisema.
"Mwanamke alizimia mara baada tu ya mapigo," alisema, akiongeza kuwa mwanaume alipiga kelele mara moja tu na baadaye akanyamaza.
chanzo:bbc

UJUMBE WA LEO:MTI WENYE MATUNDA NDIO UPIGWAO MAWE.


Sunday, 29 July 2012

UDAKU NA UDAKUZZZ:SAKATA LA CHAMELEONE


Muimbaji  chameleon  kutoka  Uganda  ni  mwizi  sana .Hapa  Uingereza  amesha tapeli watu  kishenzi  staili hio  hio na  maneja  wake. Ni  mchezo  wake.Akirudi  hapa  UK anaweza  kupigwa  mawe.Bangi  zina  msumbua  tuu.Yeye  ninani  mtu amabe  hawezi  kumuheshimu  mwakilishi  wa  Rais  wetu  Uganda   -Balozi  wetu pale  kampala.Nashanga  serikali ya  Uganda   wamemsikiliza na   kuifanya  hii  ishu  itake   kuharibu  uhusiano  mkubwa  kati  ya  nchi  hizi  mbili.Hivyo   chameleone   mnamjua  ?  juzi kawa muislam  kesho  yake  karutadi  tena .Bangi  haziwezi  zina  mpelekesha.  Anafaa   kua  jela  maana  ni  msani  jambazi.Huko  kampala  na sikia   wamesha   rushiana  risasi na  msani  Bobby  wine.  Naomba  watanzania  wote  tumzomeye  chameleon na  asirudi  tanzania  tena  kwa  tabia  yake  tena .  Hon  membe  tunaomba  hili  ulifanyie  kazi kwamba  wageni  hawezi  kuja  na  wakatu abuse  hata  nyumbani  kwetu.  Bwana  Erik   nawe  usije  uka shika  pasport  ya  mtu  ni    document  ya  serikali wala sio  mtu binafsi

MWEZI MTUKUFU: Machangu wacharazwa bakora!





Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijini.
WATUMIA BAJAJ
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.
BARABARA YA SHEKILANGO
Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.

KINONDONI
Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki

KISA KUHARIBIWA SWAUMU 
Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.


Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.
Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: “Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!”
HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?
Waumini hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.

AKINA MAMA NA BIASHARA YA NDIZI


WABUNGE MAFISADI WATAJWA:SPIKA AVUNJA KAMATI YA NISHATI, WAZIRI AELEZA WALIVYOITAFUNA TANESCO


WAKATI wabunge wakitoa tuhuma nzito dhidi ya wenzao wanaodaiwa kujihusisha na ufisadi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imebainishwa kuwa wabunge wenye tabia hiyo ni watano, watatu kutoka chama tawala CCM na wawili upinzani.

Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zimeeleza kuwa baadhi ya wabunge hao wanatoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, huku wengine wakitoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao wamedaiwa kuwa wamekuwa wakitumia nafasi zao za ubunge na ujumbe wa kamati kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi ndani ya shirika hilo la umma.

Gazeti hili limefanikiwa kupata majina ya wabunge hao, ambayo leo hatutayataja kwa sababu za kitaaluma. 

Baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni juzi na jana walisema kuwa, wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini hawapendi kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.

Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa jana na Mbunge Vita Kawawa wa Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa, Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe.

 “Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa kifungu cha 55 (3)f  mbunge au waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe. Sasa naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo," Kawawa alisema.

Aliliomba pia Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati nyingine zilizolalamikiwa kwa rushwa. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge. 

Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono Spika wa Bunge, Anne Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini.

Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.
"Ninakubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na zingine ambazo zitatajwa kwenye tuhuma hizo. Nalipeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, halafu kama ni kutajwa (wabunge hao), basi tutapata mwongozo wa kamati hiyo." alisema Spika Makinda na kuongeza:

"Nasema kwa dhati kabisa, kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge hili. Wabunge mkae vizuri. Kama kuna baadhi yetu wanaenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi, tutawezaje kuisimamia Serikali?"
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/25112-wabunge-mafisadi-watajwa.html

SUPERMODEL ALEK WEK AKISAIDI JAMII ALIPOTEMBELEA SUDAN!!




EBOLA YAZUKA TENA UGANDA!!!!


Watu kama 13 wamekufa na wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya ya Kibaale.
Chanzo cha ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.
Virusi vya Ebola havina dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni homa, kutapika, na kuhara.
Ugonjwa huo ulizuka Uganda miaka 12 iliyopita, na kuuwa watu zaidi ya 200.
chanzo:bbc

KUTOSOMA,KUTOELEWA AU KUTOJALI?


Wednesday, 25 July 2012

MOI YAELEMEWA ,WAGONJWA WALALA SAKAFUNI!!!


HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha  Taasisi ya mifupa (Moi),imeelemewa baada ya wagonjwa kufurika katika wodi na kusababisha wengi wao kulala chini na kwenye korido wakati wakipatiwa matibabu.
Mwananchi imeshuhudia baadhi ya wagonjwa katika taasisi hiyo, wakiwa wamelazwa kwenye sakafu  ndani ya wodi na wengine wakiwa kwenye korido za hospitali hiyo.

Moja ya wodi zilizoathirika na msongamano mkubwa wa ongozeko hilo la wagonjwa ni Wodi ya Sewahaji inayotumiwa na Taasisi ya Mifupa(Moi) pamoja na Hospitali ya Muhimbili.
Akizungumza na Mwananchi , msemaji wa Taasisi ya Moi, Almasi Juma alisema kufurika kwa wagonjwa katika kitengo hicho kumetokana na athari za mgomo wa madaktari uliomalizika katika siku za hivi karibuni.
“Katika kipindi cha mgomo wagonjwa waliopatiwa huduma walikuwa ni wa dharura pekee, na hivyo kupelekea kurundikano kwa wagonjwa wa kawaida,”alisema Almas na kuongeza:

“Kitengo hiki pia kinahudumia idadi kubwa ya wagonjwa wanaotokana na ajali, hali hii imechangia kwa kiasi kikubwa  kujaa kwa wodi zetu pamoja na zile tulizopewa na hospitali ya Muhimbili”.
Almasi alisema, tatizo hilo la mrundikano wa wagonjwa  linaweza kuchukua muda kidogo mpaka athiri za mgomo ziishe ndiyo hali itatengemaa na kuwa ya kawaida.

RAIS WA GHANA JOHN ATTAH MILLS AFARIKI.

Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku

Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
chanzo:bbc

Tuesday, 24 July 2012

UDAKU NA UDAKUZZZ:ZITTO AREJESHA PENZI LA WEMA NA DIAMOND!!!!!


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu.
Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.
Diamond na Wema, walinaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.
SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.
Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.
WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA?
Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.
Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.
HAKIKA WANAPENDANA
Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa!
Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema.
Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.
Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi.
Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ATEKWA ,AFARIKI!!



MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
“Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
“Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.
“Walipokwenda kuangalia wakakuta ni mtu akiwa hoi hajitambui. Baada ya kupelekwa hospitali siku ya pili alikuja mama mdogo wa marehemu Agnes aitwaye Veronica Galus na akaleta taarifa kuwa binti yao huyo amefariki dunia. Polisi tunaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika,” alisema Kenyela. Hata hivyo, kifo hicho kimeacha maswali mengi kuwa binti huyo alilishwa nini na nani?
Mzazi wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Bernad King’unza mkazi wa Kimara Dar, hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa safarini Iringa kwenye mazishi ya mpendwa wao huyo yaliyofanyika nyumbani kwao Kalenga, Iringa Julai 19, mwaka huu.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

KESI YA LULU YAPIGWA TENA KALENDA

KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, kutokana na Jaji anayeisikiliza, DK Fauz Twaib, kuwa na majukumu mengine.Akiahirisha kesi hiyo jana, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alisema Jaji DkTwaibu, anakabiliwa na majukumu mengine.

“Jaji Twaib ni Mwenyekiti wa Baraza la Kodi na pia ni Mwalimu wa Sheria katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivyo kwa sasa anatekeleza majukumu mengine katika nafasi hizo.Kwa hiyo kesi hiyo inaahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu,” alisema Msumi.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba,  yanayodaiwa kufanyika April 7 mwaka huu  nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam. 
Kabla ya kesi hiyo ya msingi haijaanza kusikilizwa, tayari imeshafikia ngazi ya Mahakama ya Rufani, baada ya kuibuka kwa utata wa umri  wa mshtakiwa huyo.

Utata huo uliiobuka baada ya mawakili wanaomtetea msanii huyo, kuomba kesi isikilizwe katika Mahakama ya Watoto kwa madai kuwa mteja wao bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama, inavyoonyesha katika hati ya mashtaka. 

Katika kesi hiyo, Lulu anatetewa na jopo la mawakili watatu, Kennedy Fungamtama (kiongozi wa jopo), Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tangantyika(TLS) Peter Kibatala na Fulgence Massawe wa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Juni 11 mwaka huu, Mahakama Kuu ilikubali maombi ya mawakili hao, kuhusu  kufanya uchunguzi wa umri sahihi wa mshtakiwa, baada ya Mahakama ya Kisutu kuyakataa.

Mahakama Kuu ilitarajiwa kuanza uchunguzi huo wa umri halali wa mshtakiwa Juni 25 mwaka huu kwa kusikiliza hoja za kila upande na kupitia vielelezo mbalimbali kuhusu umri wa mshtakiwa.

Hata hivyo hatua hiyo ilikwama na kulazimika kusimama baada ya upande wa mashtaka,  kuitaarifu mahakama kuwa, umewasilisha katika Mahakama ya Rufani,  maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu, kuhusu  kukubali kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa huyo, kama ulikuwa sahihi. 
Kwa mujibu wa kiapo kinzani, wakijibu maombi ya Jamhuri kwa Mahakama Rufani, mawakili hao wanadai kuwa Mahakama Kuu ilichukua hatua sahihi kulingana na mazingira ya kesi kwa ajili ya kutenda haki na kwamba haikupotoka katika kuamua kushughulikia suala hilo.

Vielelezo vilivyowasilishwa na upande wa mshtakiwa  katika Mahakama Kuu ni pamoja na hati za viapo vya wazazi wa mshtakiwa (mama, Lucresia Augustin Kalugila na baba, Michael Kimemeta), cheti cha kuzaliwa na cha ubatizo vya mshtakiwa vinaonyesha kuwa ana umri wa miaka 17. 

Vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16 mwaka1995  katika Kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba B.0318479 cha Julai 23 mwaka 2004. 

Lakini vielelezo ya upande wa mashtaka navyo vinaonyesha kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa zaidi ya miaka 18 yaani miaka 21.  Vielelezo ni pamoja na maelezo ya mshtakiwa huyo aliyoyatoa polisi wakati alipohojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, maombi ya hati ya kusafiria (Passport) na maombi ya leseni ya udereva.
chanzo:www.mwananchi.co.t

UKIMWI USIOSIKIA DAWA WAONGEZEKA AFRIKA!!!

Kwa muujibu wa ripoti iliyoandikwa na wataalam katika jarida la kisayansi la Lancet, hali hii imebainika baada ya watu 26,000 walioma virusi hivyo kufanyiwa utafiti.
Wataalamu hao wanasema kuwa hali hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.

Shirika moja nchini Uingereza limesema kuwa hali hiyo inazusha hofu zaidi katika bara la Afrika ambapo njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa maradhi ya Ukimwi hakuna.
Watatifi hao kutoka shirika la Afya duniani-WHO na chuo kikuu cha University College London wamegundua kuwa aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa unapatikana zaidi nchi za Afrka Mashariki.
Wataalam hao wanasema asilimia 26 % ya waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asili mia 14 katika nchi zilizo kusini mwa Afrika.
Lakini katika mataifa ya Kusini mwa Marekani , Afrika Magharibi na kati hali kama hiyo haipatikani.
Akizungumza na BBC Dr Ravindra Gupta wa shirika la UCL alisema: " virusi hivyo hambayo havisikii dawa ni kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa ipaswavyo".
chanzo bbc

HAYA NDIO MATATIZO WANAYOPATA WANAVYUO KUTOKA KWA MAPROFESA WAO!!!!!



ZANZIBAR:WAZIRI AJIUZULU NA TUME YAUNDWA



Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.
Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa watu.
Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.
Taarifa kutoka ikulu zinasemna kuwa uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja.
Chanzo:bbc

USICHOKULA WEWE MWENZIO ANAKULA!!!


Monday, 23 July 2012

WABUNGE WAMSAFISHIA ZITTO NJIA YA URAIS 2015,NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS

Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar
IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.
 
Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo. 

Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma,  Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.
 
Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.
 
"Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

"Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."  

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma,  Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.
 
Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

‘Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.
 
Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.
 Mdee amliza Zitto   
Katika hatua nyingine,  Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe’ katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.

Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa. 

‘Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee. 

Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine. 

Zitto akiri kutoa machozi 

Zitto alipulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na kushindwa kujizuia jukwaani.
  
" Kwa weli Halima Mdee aluzumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto. 

Alisema amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya Kigoma. 

Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya eneo hilo.
 
‘Wapo watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali.  Ndiyo maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.
 
Wabunge waliohudhuria
Wabunge waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni  Mdee , Amina Mwidau wa viti maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM),  Filikunjombe (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi),  Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti maalumu kutoka Pemba.

Kauli ya Nape
Alipoulizwa Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.

“Nyie andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo,” alisema Nape.
chanzo:www.mwananchi.co.t  

ARTISTS COLLABORATION - POLE ZANZIBAR [www.DarTalk.com]

MZAMIAJI AIBUA MAPYA AJALI YA MV SKAGIT!!!

Miongoni mwa wazamiaji walioshindwa kufanya kazi ya uokoaji baada ya meli ya Mv Skagit kuzama katika eneo la Chumbe na Dar es Salaam wiki iliyopita ni Muhsin Salum Muddy .

Mzamiaji huyo anasema baada ya kupinduka meli hiyo alipoteza fahamu wakati wa zoezi la kuwaokoa watu waliopata ajali hiyo.

“Sikujitambua mie, na sijui nimefikaje hospitalini hapa maana nafungua macho ndio najiona nipo katika kitanda na nimefunikwa blanketi, ninachokijua mie ni kwamba niliingia katika boti ya polisi kwenda kuwaokoa watu waliopata ajali” alisimulia kijana huyo na kuongeza:

“Pamoja na kwenda kuwaokoa walionusurika katika boti na kuchukua maiti nilikuwa na kamera kwa ajili ya kupiga picha lakini nikashindwa kufanya kazi zote kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa mbaya” alisema.

Kushindwa kufanya kazi kwa Muddy kulitokana na  mawimbi makali baharini  ambayo yalisababisha boti za uokoaji kushindwa kutulia kufanya kazi hiyo,  ambapo waokoaji wengine walikumbwa na mkasa kama wa kwake na wengine kujeruhiwa vibaya.

“Tuliondoka Bandari ya Malindi  saa 9:30 jioni na tukafika kule  saa 12 na baada ya nusu saa ndio tukawa tunaziona maiti zikielea na watu waliokuwa hai wakiomba msaada wa kuokolewa  huku wakihangaika sana na kuonyesha kuchoka, wengine tayari walishakunywa maji mengi na kuhitaji msaada lakini haikuwa rahisi kufanya kazi hiyo” alisema.

 Kutokana na hali ya bahari kuchafuka sana, baadhi ya vyombo vililazimika kurudi bila kufanya uokoaji, ambapo Muddy alisema  wenzake wengi waliokuwa ndani ya boti walitapika sana na kuishiwa nguvu.
Akisimulia tukio lililomkuta kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 30, alisema wakati wakikaribia kufika eneo la ajali chombo walichokuwa wamepanda kilipigwa na mawimbi makali na yeye kupatwa na kichefuchefu na hatimaye kutapika na kuishiwa nguvu kabisa.

Alisema wakati yeye akiwa taabani aliwaona wazamiaji wenzake wakitapika sana huku maiti na miili ya watu wanaotaka kusaidiwa wakiwa wanaonekana karibu na boti za uokoaji zilizojitokeza kufanya kazi hiyo huku baadhi ya maiti zikizagaa baharini.
Endelea kusoma hapa:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/24979-mzamiaji-aibua-mapya-ajali-ya-mv-skagit