Thursday, 31 January 2013

The udaku and udakuuzz:MWANAMKE AJIFUNGUA KAMBA YA MANILA

Akitoa ushuhuda uliowatoa machozi waumini wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyopo Kivule, Dar, Jumapili iliyopita, Lea alisema kuwa kwa muda wote huo tumbo lake lilionekana ni mjamzito.
Lea alisema, siku ya tukio alijisikia kutaka kutoa kitu kikubwa akaenda chooni kwa lengo la kujisaidia ambapo alishangaa kuona anatoa kamba ya manila, hali iliyompa hofu na kutaka kukimbia.
 “Mume wangu alikuwa nyuma ya nyumba, nilimuita ili aje kunisaidia. Alipofika alichukua kitambaa na kushika manila kisha kuanza kuivuta, ilitoka ndefu sana tena ikiwa imefungwa vifundo viwili. Ni ajabu sana,” alisema mwanamke huyo.
 Alisema siku alipofika kwenye Huduma ya WRM, Nabii Nicolaus Suguye alimwambia ametupiwa majini.
“Kwa kipindi cha miaka 31 nilikuwa siwezi kufanya kazi yoyote kutokana na maumivu makali mwilini mwangu,” alisema Lea.
chanzo:.globalpublishers

SIKILIZA VIDEO HII:Wajinga Wengi Duniani Wapo Africa; Tanzania Inaongoza

Uuzaji wasichana: Wenyeviti kikaangoni

Serikali wilayani Temeke jijini Dar es Salaam imesema itafanya uchunguzi ili kuwabaini baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa wilayani humo wanashirikiana na mawakala wanaosafirisha watoto kwenda nje ya nchi kutumikishwa.

Wenyeviti hao wanatuhumiwa kughushi barua na kuwapatia mawakala hao zikionyesha kuwa wanasafiri kihalali kwenda Zanzibar kabla ya kupelekwa Uarabuni kwa ajili ya kutumikishwa.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na NIPASHE iliyotaka kujua hatua zinazokwisha kuchukuliwa na serikali juu ya baadhi ya wenyeviti wa serikali wilayani humo wanaodaiwa kutoa barua kwa watoto wanaonunuliwa na mawakala kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchi za Uarabuni.

Mjema alisema kuwa hawezi kukataa kama wapo baadhi ya wenyeviti wanaofanya hivyo, lakini ili kupata ukweli wa jambo hilo serikali italifanyia uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Katika uchunguzi ambao umeendelea kufanywa na NIPASHE kuhusu biashara ya binadamu, imebainika kuwa watoto wanaonunuliwa na mawakala kutoka mikoani wakifikishwa Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar mawakala wanawatafutia barua kutoka kwa wenyeviti hao ili wasisumbuliwe bandarini kwahawana vitambulisho. 

Uchunguzi huo umebaini kuwa biashara hiyo iliibuka kuanzia Desemba mwaka jana na kushika kasi Januari mwaka huu na wanaosafirishwa wengi ni watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini. Wapo wachache wa kiume pia.  Uchunguzi huo ulibaini kuwa mikoa ambayo watoto hao wananunuliwa na mawakala kabla ya kusafirishwa kupelekwa nchi za Uarabuni kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za ndani ni Mtwara, Lindi, Manyara, Pwani, Tabora, Ruvuma, Tanga na Shinyanga

Askofu akemea milegezo


ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Barnabas Mtokambali, amekemea vitendo vya baadhi ya wanaume wanaovaa suruali chini ya makalio, akisema wanaofanya hivyo ni sawa na mashoga.
Alisema mwanamume kuvalia suruali chini ya makalio ni sawa na kujitangazia biashara ya ushoga ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Mtokambali alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua Chuo cha Ualimu cha Mount Sinai kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kama ilivyokuwa kwa machangudoa ambao huvaa nusu uchi kuonesha kuwa wapo katika biashara, ndivyo hivyo kwa mashoga nao wanavaa ili kujitambulisha.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, aliwaasa wanafunzi wa chuo hicho kuvaa kwa kuzingatia maadili ili wawe walimu bora kwa taifa na mfano wa kuigwa.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Alexander Chuwa, alisema licha ya chuo hicho kutoa mafunzo ya ualimu, pia kinatoa mafunzo ya elimu ya biashara na malengo ya baadaye ni kuwa chuo kikuu.
chanzo:daima

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa wezi wa pikipiki wamechomwa moto Tegeta.

Wednesday, 30 January 2013

Udaku and udakuuzzz:JACK PATRICK NUSU AUE


STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la Hafsa Sasya, Risasi Mchanganyiko linanashuka nayo.
Habari zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani ya Ukumbi  wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
CHANZO KINATIRIRIKA
Huku sharti la kutotajwa jina lake gazetini likisisitizwa na chanzo hicho, kilisema: “Unajua yule dada (Hafsa) anasoma Kurasini na anaishi Kijitonyama, namfahamu vizuri sana. Walipokutana na Jack pale ukumbini palitokea kutokuelewana kidogo.
“Baada ya muda hali ikawa sawa, watu wakajua yamekwisa. Jack akaenda zake chooni, aliporudi alikuwa na chupa na kwenda kumpiga nayo Hafsa. Mabaunsa wakamwondoa Jack ukumbini na kumwingiza Hafsa kwenye gari lake kwa lengo la kumpeleka hospitalini. Kilichoendelea hapo sijui.”
PEKUPEKU ZA RISASI
Mwandishi wetu aliingia mzigoni rasmi na kuanza kuichimba kwa kina habari hiyo ambapo alipata uhakika wa kutokea kwa tukio hilo na Jack kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alifunguliwa kesi yenye jalada namba  OB/RB/1678/13  KUJERUHI.
Baada ya kujiridhisha kwa hilo, zoezi lililofuata lilikuwa ni kuwatafuta wawili hao ili waeleze wanachokijua kuhusu tukio hilo. Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Jack.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”
HUYU HAPA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.
“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria, naamini itachukua mkondo wake.”
chanzo:globalpublisher

CHEKEEEENIIIII NA KITU KINAITWA:Idiots Of the World


Hizi ndizo picha za LULU akilia baada ya kuachiwa na mahakama





picha na kishymba.blogspot

MAONI YA JICHO LA KIJIWENI:Mbwa wa rais awe rais wa mbwa wote


BAADA ya walevi kupewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya kuandika Katiba Mpya, wamekuja na baadhi ya mapendekezo ambayo yatafanya taifa letu kuwa la pekee duniani katika utawala na ulaji bora.
Kwa vile hatukupewa nafasi kutoa maoni mbele ya Tume ya Walibora kutokana na kutokuwa na uzito wa kutosha, nimetumwa mzito wao niende kule kutoa maoni yangu na yao.
Tofauti na wazito wenzangu wenye maulaji yao, mie sitatoa maoni kama mimi bali nitawakilisha walevi wote. Pia nitakapokuwa nikitoa maoni vyombo vya umbea na habari havitaripoti kwa vile sina uzito wa kujaza kurasa zao.
Hivyo, nitatoa maoni yangu, ya bi mkubwa na walevi wenzangu. Wale walevi wakubwa watatoa maoni yao kikubwa wakati sisi tukitoa yetu kichovu. Katika kutafakari jinsi katiba inavyopaswa kuandikwa, wanakijiwe wamekuja na maoni yafuatayo:
Mosi, kama alivyosema Joni Malisera, ulaji wa rais usiguswe, tunasema uongezwe hadi kuruhusiwa kushea madaraka na bi wakubwa zake. Kama wanashea bedroom kwanini wasisheee na madaraka? Hii itasaidia kuondoa lawama kwa bi mkubwa na kufanya mambo kwa kificho.
Mfano, kama first lady atakuwa rais mwenza, hatakuwa na haja ya kujificha kwenye Asize au NGO ili kuweza kutengeneza mshiko na kupata ujiko. Hakutakuwa na malalamiko hata atakapopokewa kwa mizinga ishirini na moja na zuria jekundu.
Walevi wameona hili liwe hivi ili kuepuka matumizi mabaya ya madaraka ambapo bi mkubwa anaweza kuonekana kama mwizi na mfujaji wa madaraka na njuluku za umma asiyelindwa na katiba kama wengine. Nani anataka unyemelezi iwapo katiba inaweza kuondoa hili? Nani hapendi kuona kidosho wake aki-enjoy maulaji yake?
Pili, walevi wanapendekeza kuwa vitegemezi vya rais navyo viwe rais wa vitegemezi vyote kwenye kaya. Hata mbwa wa rais awe rais wa mbwa wote na viatu vyake viwe rais wa viatu vyote.
Hii itaondoa uwezekano wa vitegemezi kuiba sana kwa vile vinajua havina madaraka kikatiba. Pia, rais awe na mamlaka ya kutumia rasilimali zote za nchi atakavyo. Hili litaondoa kadhia kama hii tunayoshuhudia kule Ntwara ambapo badala ya kulikomboa taifa gesi inataka kulikomoa.
Tatu, walevi wanapendekeza rais kuwa anaandamana na baraza zima la mawaziri, wabunge hata marafiki na jamaa zake kwenye ziara zake ughaibuni ili kuonesha ufahari wa kaya yetu.
Pia, rais ahakikishe anatumia muda wake mwingi madarakani kufanya ziara ughaibuni ili kuomba mshiko wa kutosha kuwalisha walevi na mwingine wa kubakiza kule Uswizi kwenye akaunti zao.
Hili litaepusha watu wa karibu naye kuiba kwa tamaa wakiogopa kukamatwa kwa vile watakuwa wanalindwa na katiba. Pia, orodha ya watakaokuwa wanaandamana na rais kwenye matanuzi iwe top secret.
Uzoefu tulioupata kwa Joji Kichaka Obamiza ni walikoruhusu bangi ivutwe kisheria, ni kwamba ukihalalisha baadhi ya jinai, unapunguza ushabiki na ushiriki wake. Hivyo, kwa kuwapa maulaji kisheria walaji wote walioko mgongoni mwa rais, wataweza kula kistaarabu na si kifisi kama ilivyo sasa.
Pia, rais aruhusiwe kuandamana na waganga wa kienyeji wa kumkinga na maadui hasa usawa huu ambapo maadui wamegundua uchawi wa polonium. Hata mawaziri waruhusiwe kuweka tunguli kwenye magari na ofisini ili kufanya kazi bila hofu ya kurogwa au kupigwa zongo.

Gazeti la Risasi Ukurasa wa mbele:WEMA AMJIBU DIAMOND


Harakati za twiga........



Samaki mkunje angalii......


Lulu arejea uraiani



HATIMAYE msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, jana alipata dhamana baada ya kutimiza masharti matano aliyopewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msainii mwenzake Steven Kanumba.
Lulu alitimiza masharti hayo jana saa 9 alasiri kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Francis Kabwe.
Baada ya kutimiza masharti hayo ya dhamana, aliwaeleza waandishi wa habari huku akitokwa machozi kuwa anamshukuru Mungu, kwani yeye ndiye alifanya akapata dhamana hiyo na hivyo kumfanya atoke gerezani na kurejea kuishi uraiani.
Lulu ambaye alikuwa ameongozana na wakili wake Peter Kibatara, alisema anawashukuru wale wote waliokuwa naye bega kwa bega, tangu kesi yake ilipoanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
“Ninachoweza kusema ni kuwashukuru wale wote waliokuwa wakinihangaikia na kuniombea kwa Mungu hadi leo nimepata dhamana, narudi kuungana na familia yangu…lakini naomba watu hao waendelee kuniombea, kwani leo nimepata dhamana tu na ile kesi yangu ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijaanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi, hivyo naombeni sana waendelee kuniombea na wasinitupe,” alisema Lulu.
Msanii huyo amedhaminiwa na Florian Matungwa, ambaye anatoka Wizara ya Ardhi na Verus Mboneko Wizara ya Afya.

Msikilize Lundenga ndani- Mkasi - SO5E10

Tuesday, 29 January 2013

The udakuu and udakuzzz:MAITI YA KICHANGA YAGEUKA JOGOO


Mwananyama ni hospitali yenye hadhi ya mkoa kitabibu, ina rekodi za kuwa na matukio ya ajabu, ila hili siyo tu kwamba linaingia miongoni mwa hayo bali pia linaweza kutia fora.
Asubuhi ya Jumatano iliyopita, ilikuwa kizaazaa pale jokofu lililotumika kuhifadhi maiti ya kichanga cha mtoto, kukutwa kuna jogoo.
Mshangao zaidi ni kwamba ndani ya lile jokofu, pembeni ya yule jogoo, kulikuwa na hirizi pamoja na tunguri.
TUKIO LILIKUWA HIVI
Habari kutoka vyanzo vyetu, zimewekwa wazi kuwa Jumanne iliyopita, saa 7 mchana, polisi walipigiwa simu, wakataarifiwa kuhusu maiti ya mtoto iliyokuwa imetelekezwa eneo la Kigogo, Mbuyuni, Dar es Salaam.
Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta maiti hiyo ya kichanga ikiwa imefunikwa kwa kuzungushiwa sanda.
ETI, KILIKUWA KICHANGA CHA KIKE
Kwa mujibu wa Moses Madilu, mkazi wa Kigogo, aliyedai kushuhudia tukio hilo, polisi walipofika eneo la tukio waliikagua maiti hiyo na kubaini kwamba ni ya kike.
Chanzo chetu kikaeleza kuwa baadhi ya mashuhuda, hususan wanawake, walitokwa na machozi kwa masikitiko kwamba itakuwa mtu alijifungua halafu akakinyonga kichanga hicho kabla ya kukitelekeza eneo hilo.
“Baada ya kujiridhisha kwa kazi yao, polisi waliichukua maiti hiyo ya kichanga, wakaipakia kwenye ‘difenda’, wakaipeleka Hospitali ya Mwananyamala,” kilieleza chanzo chetu.
HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ndani ya hospitali hiyo, mwandishi wetu alielezwa kuwa polisi walipofika, walishusha maiti hiyo na kumkabidhi mganga wa zamu aliyejulikana kwa jina moja la Dk. Liwa.
Muuguzi mmoja wa hospitali hiyo (jina tunalo) alisema: “Dk. Liwa aliwaambia wale polisi wapeleke maiti hiyo mochwari.
“Polisi walifanya hivyo lakini kule mochwari walimkuta msimamizi mkuu, Omar Buyoya aliyekataa kuipokea kwa vile daktari hakuthibitisha kama kile kichanga kilikufa au kilikuwa hai.
“Polisi na Buyoya walivutana kwa muda mrefu, alitokea mhudumu mwingine wa mochwari aliyekuwa akijuana na polisi mmoja aliyebeba ile maiti, alikubali kuupokea mwili huo na kuingiza ndani kwenye jokofu la kuhifadhia maiti.”
Muuguzi huyo aliendelea kusema kuwa siku iliyofuata, Dk. Liwa alifika mochwari na alipofungua jokofu na kufunua sanda, badala ya kukuta maiti ya kichanga, alikuta jogoo, tunguri na hirizi.
Dk.Liwa alipatwa  na mshangao mkubwa huku jasho likimtoka kutokana na uoga, aliwaita wafanyakazi ambao walijazana hapo  mochwari kushuhudia.
“Baadhi ya wafanyakazi walipigwa na butwaa huku wengine wakicheka hadi kudondoka chini na wakawa wanajiuliza kama kweli polisi wanaweza kupeleka jogoo hospitali au ni mambo ya kishirikina,” alisema muuguzi huyo.
Dk. Liwa na wafanyakazi wenzake waliondoka mochwari na kuacha hilo jogoo katika chumba cha maiti huku wakishindwa la kufanya.
MGANGA MKUU ANENA
Gazeti hili lilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani ambaye alikiri  kuonekana kwa jogoo badala ya maiti ya kichanga.
“Polisi walituletea kifurushi wakiamini kuwa ni maiti ya kitoto kichanga ambapo tulikipokea lakini ilipotazamwa na daktari, tulikuta jogoo, hirizi na tunguri, tuliamua kumchoma moto kwa sababu kile nichumba cha kuhifadhi maiti siyo cha kuhifadhia mizoga ya kuku, ng’ombe au mbwa,” alisema Dk. Ngonyani.
POLISI WANENA
Naye Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kwamba wao kama jeshi la polisi walipigiwa simu na raia mwema kuwa  kuna maiti ya kichanga ambapo askari waliondoka hadi eneo la tukio na kuichukua mpaka Hospitali ya Mwananyamala.
“Polisi waliichukua hadi Hospitali ya Mwananyamala kwa wataalamu na baada ya kuikabidhi waliondoka na kuendelea na shughuli nyingine, nami nashangaa kusikia kwamba madaktari walikuta bonge la jogoo,” alisema Kenyela.
MASWALI MATANO
Je, ni kweli polisi waliikagua maiti na kugundua ni kichanga cha kike?
Kama ndiyo, ilikuwaje kikageuka jogoo?
Kwa nini daktari hakuipima ile maiti, badala yake akaelekeza ipelekwe mochwari?
Je, au polisi walibeba mzoga wa jogoo, wakampakia kwenye difenda wakidhani ni maiti ya kichanga?
Mkweli nani, polisi wanaodai kupeleka maiti ya kichanga, au hospitali wanaosema walipelekewa mzoga wa kuku, tunguri na hirizi?
chanzo:globalpublishers.

Photo la leo: nani zaidi?



Soma ujumbe kutoka kwa wajumbe!!!


Hatari: Wasichana wauzwa kama njugu

Biashara ya binadamu imeibuka kwa kasi nchini na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri kati ya miaka 8-15 baadhi yao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  kusafirishwa kinyemela kwenda katika nchi za Uarabuni.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na NIPASHE kwa takribani wiki mbili, umebaini kuwa biashara hiyo imeibuka kuanzia Desemba mwaka jana na imeshika kasi Januari mwaka huu na wanaosafirishwa  wengi ni watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini. Wapo wachache wa kiume pia.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, alipoulizwa na NIPASHE alithibitisha kupata taarifa za kuwapo kwa biashara hiyo ingawa alisema kuwa hana takwimu za watoto ambao wamekamatwa wakitaka kusafirishwa.

“Tatizo la kusafirisha watoto lipo, lakini nina watu ambao wanashughulikia suala hilo pale bandarini, nitafute kesho (leo) nitakupa takwimu zote kuhusiana na biashara hiyo baada ya kuwasiliana na watu wangu,” alisema Kamanda Kanga.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa mikoa ambayo watoto hao wananunuliwa na mawakala maalum kabla ya kusafirishwa kupelekwa nchi za Uarabuni kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za ndani ni Mtwara, Lindi, Manyara, Pwani, Tabora, Ruvuma, Tanga na Shinyanga.

Mtoto wa Karume alipuliwa Zanzibar


MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni (CCM), Salmin Awadh Salmin, amesema ameshagazwa na mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Shumbana Amani Karume, kuungiwa umeme bure na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Alitoa tuhuma hizo wakati akichangia ripoti ya uchunguzi kuhusu ubadhirifu katika shirika hilo iliyowasilishwa na mwenyekiti Kamati ya Kuchunguza Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma, Ali Omar Shehe.
Awadh alisema kwamba kitendo cha kumuungia umeme bure mtoto huyo wa kiongozi mstaafu katika kitega uchumi chake ni kwenda kinyume na misingi ya utawala bora Zanzibar.
Alisema kwa mujibu wa ripoti ya PAC, mtoto huyo aliungiwa umeme bure na kutumika nguzo 31 kuvuta umeme kutoka umbali wa kilomita 2.5 wakati wananchi wanyonge wamekuwa wakitozwa gharama Zanzibar.
Alisema kwamba kitendo hicho lazima kipigwe vita kwa sababu kimelenga kuitafuna nchi na kuvuruga misingi ya utawala bora.
chanzo:daima

Mzimu wa gesi wazidi kumtesa Rais Kikwete


MOTO wa gesi asilia unazidi kumwakia Rais Jakaya Kikwete, ambapo vyama mbalimbali vya siasa na viongozi wakuu wa dini nchini wameendelea kumtaka kiongozi huyo avunje ukimya na kuingilia kati.
Wakati hali ikiwa tete huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijaribu kusaka suluhu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Askofu Mkuu wa Anglikana nchini, wametoka msimamo mzito kuhusu sakata hilo.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, jana alitoa msimamo wa chama chake kwenye kikao cha dharura cha Baraza Kuu, akisema wako pamoja na wananchi wa Mtwara na kwamba serikali inapaswa kusikiliza sauti yao.
Wao CUF kupitia kwa Waziri wao wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Mapinduzi ya Zanzibar, Juma Haji Duni, alisema mauaji ya raia wema wanaodai haki yao ya gesi asilia yanayofanywa na polisi hayakubaliki.
Yeye Askofu Valentino Mokiwa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha ukimya na badala yake asitishe ziara zake nje ya nchi aende Mtwara kusikiliza kilio chao na kupata ufumbuzi wa haraka.
Akifungua kikao cha Baraza Kuu, Mbowe alisema ni wakati wa serikali kusitisha mara moja mpango huo wa kusafirisha gesi hiyo kwenda Dar es Salaam na ikae na wananchi kwa ajili ya kupatia ufumbuzi.
“Haya yanayotokea leo mkoani Mtwara ni matokeo ya wananchi kuchoka na ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM, wanachofanya Mtwara sio jambo la kusifu ila ni ujasiri wa kupongezwa,” alisema.
Alisema serikali ya CCM kwa sasa inapaswa kujiandaa kutoa maelezo ya mrejesho wa madini katika maeneo mbalimbali ya nchi, usafirishwaji wa meno ya tembo pamoja kuweka wazi mikataba zaidi ya 26 katika sekta ya uchimbaji wa gesi nchini.
Mbowe alisisitiza kuwa serikali haiwezi kuwa na nia ya dhati ya kuwasikiliza wananchi kwa kuwa miongoni mwa wamiliki wa makampuni yanayochimba gesi ni ya viongozi wa CCM ikiwemo Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana kupitia makampuni hayo (Artimax).
Mbali na Kinana Mbowe pia alimtaja kiongozi mwingine wa CCM mwenye maslahi binafsi katika gesi kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, ambaye pia ni Mbunge wa Newala.
“Wakati wa kubembelezana katika kutekeleza wajibu kwa wananchi umepitwa na wakati na suala la wananchi kudai rasilimali ziwanufaishe halitaishia Mtwara pekee bali litaenda kila eneo nchi nzima,” alisema.
Duni asema yahusuyo CUF

Furaha ya msanii Lulu kurejea uraiani yayeyuka...

Monday, 28 January 2013

Wema sepetu na enziiii zilee aliposhinda u misss





Mahakama yakubari kumuachia LULU endapo wadhamini wawili watakiwa kuwa na Sh20m kila mmoja


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempatia dhamana msanii wa Filamu Elizabeth Michael (Lulu) kwa masharti ya kupata wadhamini wawili wanaofanya kazi Serikalini wakiwa na Sh 20milioni kila mmoja.

MWeee uchawi au kuloga kazii kweli kweli!!!!!

Baadhi ya picha ya ajali ya moto iliyoua watu 245 BRAZIL








Video ya Watu 245 wapoteza maisha ndani ya ukumbi wadisco

Kama MwanaHalisi ni wachochezi, Mwigulu na Mkama ni kina nani?


JULAI 30, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ililifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi.
Kwa mujibu wa serikali, sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi, likiwa na nia ya kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola, hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.
Katika tamko la serikali lililotolewa na Msajili wa Magazeti, Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia lilichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
Nimelazimika kufukunyua hilo leo ili kukumbushana juu ya uonevu dhidi ya baadhi ya vyombo vya habari, hasa vile vinavyoonekana kusimama katika ukweli huku viongozi wanaotoa uchochezi wakiachwa.
Kati ya matoleo ya gazeti hilo yanayolalamikiwa na serikali kuwa yameleta uchochezi, ni lile lililokuwa na kichwa cha habari kinachosema ‘Aliyemteka Ulimboka ni huyu hapa’. Sikutegemea wala kuamini kuwa nchi inayodai kusimama katika demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, ingeweza kuchukua hatua ya kuamua kukizima chombo hicho ili kisiendelee kufukunyua yale ambayo yamekuwa yakitendwa ovyo na baadhi ya watendaji wa serikali.
Hivi kweli serikali makini imeshindwa kuyafanyia kazi yale yaliyoandikwa na gazeti hilo na badala yake haitaki kuchokonolewa ikalazimika kulifunga gazeti hilo kwa kipindi kisichojulikana?
Sitaki kuafiki wala kukubaliana na hatua hiyo ya kimabavu. Hivi sasa japo kuna taarifa nyingi mbaya na za kichochezi zinatolewa na baadhi ya viongozi wa vyama, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Ajali ya magari matatu yaua 3 Shinyanga.

Kikwete rudi umalize ugomvi wa gesi Mtwara


MZOZO wa gesi mkoani Mtwara umefika mahali pabaya na serikali lazima ielekeze nguvu zake huko kuhakikisha mzozo huo unamalizika.
Kwa takriban wiki mbili sasa, vyombo vingi vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa mbalimbali kueleza jinsi wananchi wa Mtwara wasivyoridhika na uamuzi wa serikali kujenga bomba la gesi kutoka mkoani humo kuja jijini Dar es Salaam bila kuwaambia wao watanufaika vipi.
Mengi yameandikwa na p engine serikali haikuona uzito, lakini baada ya tukio la jana, tunadhani ni wakati muafaka sasa kuamka na kulishughulikia jambo hili ili kurejesha amani Mtwara.
Hatuna nia ya kurejea kila kitu kilichotokea kwenye vurugu za jana, lakini kwa kifupi ni kwamba nyumba, magari na mali nyingine za wabunge, Anna Abdallah (Viti Maalumu) na Mbunge wa Masasi, Mariam Kasembe, wote wa CCM, zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya wananchi.
Wabunge hao wamekumbwa na mkasa huo kwa madai kuwa ni wasaliti, eti wameungana na serikali ya Rais Kikwete kuwahujumu juu ya gesi yao.
Uharibifu mwingine uliofanywa katika vurugu hizo ni pamoja na kuchoma majengo ya serikali, vituo vya Polisi na kusababisha vifo vya watu wanne, akiwemo askari polisi mmoja.

Sunday, 27 January 2013

Elimu haina mwisho,huyu ndio yule babu wa miaka 88 aliyejiunga shule ya msingi!!!!!!

Siri vurumai zinazoendelea nchini yafichuka


 Siri ya vurumai zinazoendelea nchini imefichuka kwa kile kinachoelezwa kuwa ni matokeo ya umma kukosa imani na serikali.
Mwanasiasa mkongwe Augustine Mrema , amesema vurumai zinazoendelea nchini ni matokeo ya umma kukosa imani na serikali.
Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam alisema, raia hawana imani na jinsi nchi inavyoendeshwa kutokana na serikali kufanya mambo kiholela kupindukia.
Alisema viongozi na vyombo vya kuhudumia wananchi havitendi haki vinakandamiza wanyonge na kuendesha serikali bila umakini.
Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika awamu ya pili, alisema kuonyesha kuchoka wananchi wanajichukulia sheria mkononi.
chanzo:nipashe

Polisi watumia risasi za moto kufuatia vurugu Dumila..

Wanafunzi wa kike wakumbwa na ugonjwa wa ajabu


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya De Paul inayomilikiwa na Kanisa la Katoliki jimbo kuu la Mbinga mkoani Ruvuma wamekumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuweweseka na kupooza viungo.
Habari zilizopatikana jana kutoka kwenye shule hiyo zimesema kuwa siku tatu zilizopita dalili zilianza kuonekana kwa baadhi ya wanafunzi ambao baadae hali zao ziliendelea kuwa mbaya na uongozi wa shule ulilazimika kuwakimbiza kwenye hospitali kwa matibabu.
Wanafunzi tisa walikumbwa na ugonjwa huo wa kuweweseka na kupooza baadhi ya viungo vya miili yao.
Habari zaidi ambazo zimeelezwa na baadhi ya wanafunzi na walimu ambao wameomba majina yao yahifadhiwe, zilisema kuwa siku ya pili wanafunzi wengine saba walibainika kuwa na tatizo hilo na kupelekwa katika hospitali ya serikali ya wilaya kwa matibabu.
Jitihada za kuupata uongozi wa shule hiyo ziligonga mwamba baada ya kutopatikana kwa simu zao za mikononi.
NIPASHE ilimpata Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Dk. Damas Kayela, ambaye alikiri kuwapokea wanafunzi 16.
Dk. Kayela alisema kuwa baada ya kuwapokea wagonjwa hao, jopo la madaktari lilianza kuwahudumia kwa kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na matatizo yaliyokuwa yanawakabiri lakini baadae jopo la madaktari lililazimika kwenda kwenye eneo la shule ya De Paul ambapo walipofika waliwakuta wanafunzi wengine sita wakiwa wanasumbuliwa na tatizo hilo. Baadaye iligundulika kuwa tatizo lililowakumba wanafunzi hao ni la ugonjwa wa kuchanganyikiwa na kulegea mwili.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alithibitisha kuwa wanafunzi 22 wa shule hiyo waligungulika kuwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa na kulegea mwili na kwamba kwa sasa wataalamu wa afya wakiwemo madaktari walishakwenda kwenye shule hiyo kutoa ushauri zaidi kwa wanafunzi na uongozi wa shule hiyo.
chanzo:nipashe

Friday, 25 January 2013

The udakuu and udakuuzzz:Machangudoa wawaomba wateja wao kuwa na subira,biashara hawatoicha ng'oooooooo!!!!


BAADHI ya akinadada wanaofanya biashara haramu ya kujiuza katika maeneo ya Jiji la Dar, wameeleza kuwa licha ya kupewa kashikashi na jeshi la polisi na wakati mwingine kukamatwa na kupelekwa mahakamani, hawawezi kuiacha ‘kazi’ hiyo kutokana na ugumu wa maisha.
Wadada hao waliyasema hayo, baada ya kunaswa na paparazi  maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku  chache baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara hiyo ndiyo maisha yao.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.
“Nani asiyependa kulala usiku na familia yake? Ukituona barabarani ujue hali ni mbaya. Hata kama polisi wanatukamata lakini wanatuachia na tunarudi sokoni kama kawaida,” alisema changu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuena na kuongeza:
“Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.”
Katika hali ya kushangaza wakati changudoa huyo akizungumza hayo, wapo waliokuwa wakimshawishi paparazi  anunue ngono kwa maelezo kuwa, hali ni mbaya kwani polisi wamekuwa wakifanya doria mara kwa mara.
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.
Hata hivyo, katika pitapita ya mwandishi  maeneo mengi kama vile Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila mteja anayewatokea.
chanzo:globalpublishers

Hili ndilo songiii la KEISHA ft. Diamond (NIMECHOKA) - OFFICIAL VIDEO

JK amponza ofisa usalama


MTU mmoja anayedaiwa kuwa ni ofisa usalama wa taifa, amenusurika kuuawa na wananchi wa kijiji cha Msimbati, kata ya Madimba, wilayani Mtwara, akidaiwa kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete kutaka kumrubuni mkuu wa kaya ya Wasimbati abadili msimamo wake kwenye sakata la gesi.
Hivi karibuni mkuu huyo wa Wasimbati, Somoe Mtiti (106), aliionya serikali kuwa endapo italazimisha kusafirisha gesi kutoka Mtwara bila maridhiano na wananchi, ingelifika Dar es Salaam ikiwa maji.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyefika kijijini hapo jana kufuatilia tukio hilo, shangazi wa mtuhumiwa, Fatuma Tom, alikiri kijana wake Seleman Babu kufika kijini hapo juzi saa 10 alasiri na kumwomba ampeleke kwa bibi yule mkuu wa kaya.
Fatuma alisema kuwa kijana wake Babu ni ofisa usalama wa taifa anayefanya kazi jijini Dar es Salaam na kwamba alimsindikiza hadi kwa bibi huyo ambapo baada ya kufika, alimweleza kuwa ametumwa kwake na viongozi wa juu aondoke naye kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na Rais Kikwete na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia.
Fatuma alisema kuwa bibi yule alikataa maelezo hayo licha ya Babu kumshawishi sana akisema kama hawezi kuondoka wakati huo kuna gari ingelimpitia Jumanne ijayo.
“Kadiri mabishano yalivyozidi walinzi wa bibi waliingilia kati huku wananchi wakizidi kukusanyika na hivyo kumtaka kijana wangu aondoke, lakini akawa anabisha,” alisema.
Kadiri watu walivyoongezeka, hali ilibadilika na kuanza kumrushia mawe kijana yule aliyekimbilia kwenye gari lake lenye namba za usajili T609 PXG aina ya Mark II na kuondoka kwa kasi, lakini kwa kuwa ni mgeni na njia alijikuta akikwama, hivyo kufungua mlango na kutimua mbio.
Shangazi huyo aliongeza kuwa wananchi waliendelea kuliponda gari hilo kwa mawe kisha kuliteketeza kwa moto wakiwa wamekasirishwa na hatua hiyo ya kijana huyo wakitafsiri kuwa ni mpango wa serikali kutaka kumuua mkuu wao wa kaya ili wafanikishe malengo yao ya kupeleka gesi Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Salum Athuman, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba gari alilokuwa akitumia Babu, ni mali ya mdogo wake Mussa Babu kwa mujibu wa vielelezo walivyovikuta ndani ya gari hilo.
kushuhudia masalia ya gari hilo, Babu alipotafutwa kwa simu, alikana kushambuliwa akidai hajawahi kwenda huko siku za karibuni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mary Nzuki, alisema kuwa Babu hajaenda polisi kulalamika hivyo hawana taarifa za kushambuliwa kwake.
Bibi Somoe amekuwa maarufu sana kijijini hapo kiasa cha uongozi kumwekea ulinzi kutokana na uwezo aliouonesha mwaka 2005 wakati wa uchimbaji wa gesi, alipoitwa na makampuni kuyasaidia baada ya mitambo yao kugoma kushuka chini wala kupanda juu.
Inaelezwa kuwa baada ya bibi huyo kufanya tambiko katika mitambo hiyo ndipo ikaanza kufanya kazi yake kama kawaida, hivyo tishio lake kwa serikali kuhusu sakata la gesi linaloendelea liliwatisha viongozi wa serikali.
chanzo:daima

Video ya watoto wakicheza miondoko ya Azonto!!!!!!

Kesi ya mtawa kupora mume wa mtu yatajwa


KESI  ya  madai  inayomkabili aliyekuwa  Mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani anayedaiwa kufumaniwa na mume wa mtu imepangwa  kusikilizwa Januari 29 mwaka huu.
“Sista’ Yasita  licha ya kuwa mtumishi  wa afya katika  Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa  lakini inadaiwa  ameachana  na maisha  ya  kitawa  miaka  miwili  iliyopita kwa hiyari yake akiwa Mtawa  wa Shirika la  Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMA).
Shauri  hilo  la madai  linatarajiwa  kuanza kusikiliza  katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa, mbele ya Hakimu  Jaffari  Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh3 milioni baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa aitwaye  Martin Msangawale (39), Mhasibu wa Manispaa ya  Sumbawanga.
Siku hiyo  ya kusikilizwa kwa shauri  hilo  mlalamikaji  katika  shauri  hilo  Asteria  anatarajiwa  kuwaleta  mashahidi wake  wanne mahakamani hapo.
Katika hati ya  awali  ya madai inadaiwa kuwa mshtakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe  Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Chipu iliyoko eneo la Katandala mjini Sumbawanga usiku wa  Desemba 24 mwaka  jana siku ya mkesha wa  Sikukuu  ya Krismasi. Hakimu, Mkinga  alisema kuwa  kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe Januari 21 imeahirishwa hadi  Januari 29 mwaka huu ili kumapatia  mlalamikaji muda wa  kuwaleta  mashahidi wake mahakamani.
Mlalamikaji  wa shauri  hilo la madai, Asteria  amedai  nje  ya mahakama kuwa alifunga ndoa  ya Kikristu  na mumewe  huyo Martin Msangawale  mwaka 2007.
Kesi hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi hususani wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake kutokana na kuwa gumzo kubwa na kuteka hisia za watu wengi hivi sasa
chanzo:mwnanchi

Happy birthday my shostiii JENNIFER LIVIGHA!!!


This is your special day, 
It has finally come your way! 
I wish you to be happy whatever you do,
And your bday to be lovely - exactly like you!

                                                                    Much lovee  from mama j2

Vipindi vya mapenzi mchana! Serikali iko wapi?????


KUNA baadhi ya matukio yamekuwa yakitangazwa kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ambayo kwa kweli msingi wake ni kuipotosha jamii.
Matukio hayo yamekuwa yakitangazwa na baadhi ya vituo vya redio, ambazo wakati mwingine unaweza kujiuliza ni maadili gani ya kazi wamejifunza wahusika katika vyuo vya uandishi wa habari walivyosoma.
Baadhi ya vipindi vya vituo hivyo, vimekuwa kero kutokana kutojali matangazo yao yanawalenga wasikilizaji wa rika gani.
Kwa kawaida, kuna vipindi ambavyo havipaswi kusikilizwa au kuonwa na watoto, ndiyo maana vinatakiwa kutangazwa usiku wakati watoto wakiwa wamelala.
Lakini kutokana na mfumo wa utandawazi, siku hizi baadhi ya vituo hivyo havijali tena maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Hali hiyo ya kutangaza vipindi bila kujali utamaduni wa Watanzania, imekuwa ikilaaniwa na baadhi ya wazazi, ingawa vituo hivyo haviko tayari kubadilika hadi sasa.
Matangazo yanayolalamikiwa na baadhi ya wananchi ni kuhusiana na mazungumzo ya matendo ya mapenzi, ambayo kiukweli siwezi kuyataja hapa.
Mambo ya mapenzi kwa kawaida yana muda wake na kwa siri, hivyo ni ajabu kusikia baadhi ya vituo hivyo vya redio kuyatangaza hadharani.
Vipindi hivyo vimekuwa vikitaja baadhi ya matendo yanayofanywa na watu wa jinsia mbili tofauti katika mapenzi, mchana kweupe!
Chuki kutoka kwa watu wasiopendelea utaratibu huo, hujitokeza zaidi kwenye vyombo vya usafiri wa umma kama vile daladala, ambako hupanda watu wa rika mbalimbali ikiwemo watoto wadogo.
Kuna vitu vimekuwa vikizungumzwa, kiukweli havipaswi kuzungumzwa katika mazingira kama hayo ya mchanganyiko wa watu.
Ukiangalia vipindi hivyo, havina mafundisho yoyote zaidi kuwapotosha watoto wanaovisikiliza.
Niliwahi kudadisi, labda inakuwaje vipindi hivyo vimekuwa vikiachiwa hewani bila kuchujwa, lakini inaelezwa kuwa huu ni wakati wa soko huria, hivyo kila kinachofanywa, lengo ni biashara zaidi.
Aidha, wapo wanaodhani kuwa, mapenzi siku hizi yamekuwa burudani, hivyo katika vituo hivyo matangazo hayo ni moja ya njia ya kuwavutia wateja zaidi. Vipindi hivyo vinazidi kuongezeka kila kukicha.
Waganga wa jadi pia nao hujitokeza kununua vipindi kwa ajili ya kutangaza biashara zao za dawa za kuimarisha mapenzi na kudumisha ndoa.

Hivi ndivyo wanafunzi wa chuo cha St. John Dodoma walivyondamana..

Thursday, 24 January 2013

AIBU YA MKE WA MTU KUCHOJOA NGUO ZOTE KWA UTAMU WA BENDI!!!



KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza, Amani linakumegea kilichotokea.
Katika onesho hilo, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu alifanya kitendo cha aibu baada ya kusaula nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.
Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.
Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo (jina lake halikupatikana) alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.
Mpigapicha  alipojaribu kumpiga picha dada huyo alihamaki na kumjia juu huku kumtishia kumvunjia kamera yake huku akidai kuwa yeye ni mke wa mtu, hivyo hapaswi kupigwa picha.
“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,” alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake  moja baada ya nyingine.
Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye  aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita  kwa jina la wifi.
“Wifiii…, wifiii…, weee wifii pombe gani hizo, usivue nguo, usifanye hivyo ni aibu,  itakuwaje kaka akiziona hizo picha magazetini?” alisema dada huyo aliyedaiwa kuwa ni wifi mtu lakini pamoja na kumpigia kelele hizo haikusaidia kumzuia  mwanamke huyo mcharuko kusaula nguo zake.
Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.
Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya  kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.
Chanzo:globalpublishers

BURUDIKA MOVIE: MY ANGLE. (Bongo film)

Kiwanda cha Mchina chaua wanne mjini Kibaha

Watu wanne wamefariki dunia katika mlipuko unaodaiwa kuwa ni wa bomu ambao umetokea kwenye kiwanda cha Hong Yu Steel cha kuyeyusha vyuma chakavu kilichopo Zogoani, katika mji wa Kibaha.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema tukio hilo lilitokea juzi na kwamba ni mlipuko uliosababishwa na ajali ya kawaida.

Alisema tayari mabaki ya vyuma vilivyolipuka yamepelekwa kwa wataalam wa milipuko kwa uchunguzi zaidi na kwamba taarifa zitatolewa baadaye.

Matei alisema mlipuko huo ulitokea wakati uyeyushaji wa vyuma ukiendelea na kwamba hiyo ni ajali ya kawaida.

“Hatuwezi kusema sasa kwamba ni bomu kwa sababu kwanza madhara yametokea tu kwa binadamu, bomu lingeweza kuvunja kuta na paa. 

Hii ni makavu kwa ndugu wooooooooooooooote.

Wanavyuo waongoza kwa ukahaba


WANAFUNZI wa vyuo vikuu, hasa vya Dar es Salaam, Mkwawa Iringa na Chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam, vimeonekana kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofanya biashara ya ngono kuliko vyuo vingine nchini.
Hayo yalibainishwa na Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi wa Manispaa ya Iringa, Gaspar Nsanye, alipozungumza na wadau mbalimbali katika mdahalo wa siku mbili kuhusu mpango mkakati wa AMICAAL kuhusu makundi yaliyosahaulika katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na ukimwi na kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo, madiwani, wakurugenzi na wadau waliopo mkoani hapa.
Alisema matokeo ya zoezi la kupata maoni na hali halisi ya makundi maalumu yalionesha kuwa baadhi ya makundi yapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya mashoga, wanaotumia dawa za kulevya, watoto wa mitaani, wafungwa pamoja na wanaofanya biashara ya ngono.
“Hivi sasa kuna kasi kubwa ya kukua kwa makundi hayo na yanaelekea maeneo mengine hasa mijini na idadi ya watu wanaopata maambukizi mapya katika makundi haya inaongezeka,” alisema Nsanye.
Alisema sababu hasa zilizotajwa za watu kujiingiza katika makundi hatarishi ni pamoja na utamaduni katika baadhi ya maeneo kama Tanga na Zanzibar, umaskini na matatizo hasa kwa wafungwa, uchangiaji wa vifaa kwa wanaojidunga dawa za kulevya na ngono isiyo salama.
Alisema miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Manispaa ya Iringa ni kuongezwa kwa vituo vya huduma ya afya kwa walioathirika na dawa za kulevya na ukimwi na kutoa elimu jinsi ya kufanya ngono salama, kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya kondomu kwa watumishi, wanafunzi, vijana na kusambaza kondomu kwenye baa, kata vyuoni na katika jamii.
chanzo:daima

Wednesday, 23 January 2013

MWEEEEE sikiliza maneno ya MWANAUME WAKINIGERIA anapokutana na mwanamke mrembo!!!!!!!

Muingereza ahukumiwa kifo Indonesia


Lindsay Sandiford alikamatwa mwezi Mei mwaka jana baada ya polisi mjini Bali waliokuwa wanafanya ukaguzi wa mizigo kupata kilo 4.8 za cocaine katika mzigo wake.
Sandiford, ambaye anwani yake nchini Uingereza ni Gloucestershire, alisema kuwa alilazimishwa kubeba mzigo huo kuuleta kisiwani Bali.
Wakili wake alisema kuwa waligutushwa na hukumu iliyotolewa na kwamba watakata rufaa.

Sandiford alikamatwa akiwa safarini kutoka Bangkok kuelekea Thailand.

Palikuwa na mshangao mkubwa katika mahakama wakati hukumu ilipotolewa.
Ingawa adhabu ya ulanguzi wa madawa ya kulevya nchini Indoesia ni hukumu ya kunyongwa, upande wa mashtaka ulikuwa umeomba apewe miaka kumi na tano gerezani wakisema kuwa umri wake unapaswa kuwa kigezo cha hukumu ambayo ingetolewa na kwamba hakuwahi kuhusishwa na kashfa zengine.
Lakini wakitoa hukumu hiyo, majaji walisema kuwa utetezi wao haukuwashawishi kuweza kupunguza hukumu hiyo.
Waliongeza kuwa Bi Sandiford hakuonekana kujali kuhusu athari za kitendo chake.
Akiondoka mahakamani, mama huyo kutoka Gloucestershire alionekana kupigwa na mshangao , akifunika uso wake kwa kitambaa.
Wakili wake alisema lazima atakata rufaa. Aliongeza kuwa ni nadra kwa majaji kutoa hukumu kama hiyo kinyume na adhabu iliyokuwa imependekezwa na upande wa mashtaka.
Majaji hata hivyo walisisitiza kuwa Sandiford ameharibu sifa ya Bali kama mji wa kitalii na kuhujumu sheria ya serikali dhidi ya madawa ya kulevya.
Bi Sandiford anatuhumiwa kuwa mmoja wa genge la waingereza watatu wanaohusika na ulanguzi wa madawa ya kulevya.
chanzo:bbc