KAMPUNI ya Kichina ya Chico imeanza kubomoa na kujenga upya kipande cha barabara ya lami kati ya Shelui na Mlima Sekenke, mkoani Singida chenye urefu wa zaidi ya kilomita 33.
Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Singida baada ya kukagua eneo hilo jana, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema kampuni hiyo inatakiwa kubomoa na kujenga upya kipande hicho kwa gharama zake yenyewe, baada ya uchunguzi uliofanywa kuonyesha ujenzi ulifanyika chini ya kiwango.
Dk Magufuli alisema barabara hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya Sh35 bilioni mwaka 2008 zikiwa mkopo, ilitarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 15 lakini imebomoka kipindi kifupi.
Dk Magufuli alisema serikali imechukua hatua hiyo ili kutoa fundisho kwa kampuni nyingine zinazoteleleza miradi chini ya kiwango na kusababisha hasara kwa Watanzania.
Alitoa onyo kwa makandarasi washauri na wahandisi wanaopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo, kuwa makini.
Kwa mujibu wa mkataba ujenzi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya Januari 30, mwakani.
Kwa mujibu wa mkataba ujenzi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya Januari 30, mwakani.
chanzo:mwananchi
No comments:
Post a Comment