WIVU wa mapenzi umemsababishia madhara Christina Nakamwela (38) mkazi wa Kijiji cha Sinyanga, Kata ya Ipande wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kwa kutobolewa macho yake na mumewe, Benard Mbembele.
Akisimulia mkasa huo, baba mzazi wa mwanamke huyo, Andason Nakamwela, alisema kuwa mtoto wake alipatwa na mkasa huo juzi saa 2:00 usiku baada ya mumewe kutoka kunywa pombe na kuanza kumuadhibu akimtuhumu kuwa alichelewa kupika kwa sababu alikuwa kwa mwanaume mwingine.
Alieleza kuwa baada ya kubishana kwa takribani nusu saa, ndipo mwanaume huyo alianza kumpiga mkewe kwa vitu vyenye ncha kali maeneo ya kichwani na hivyo kumjeruhi kisha kumtoboa macho yote mawili.
Nakamwela alifafanua kuwa, ugonvi huo uliamuliwa na mwenyekiti wa kijiji hicho, baada ya kusikia mayowe.
Alisema kuwa alipewa taarifa na mwenyekiti huyo baada ya tukio hilo na hivyo kulazimika kukodi usafiri na kumkimbiza mwanae katika hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa ajili ya matibabu.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Frank Mbembele alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa, kijana huyo alidhamiria kumuua mkewe kwa kuwa alikuwa akimpiga kwa kutumia kitu chenye ncha kali maeneo ya usoni.
Alibainisha kuwa, alitumia taratibu za kisheria kwa kuwaagiza mgambo wamkamate mtuhumiwa na kumfikisha katika kituo cha polisi cha wilaya ambako anashikiliwa hadi sasa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Apasaria Lumisha, alikiri kumpokea mgonjwa huyo na kwamba juhudi zinafanywa ili kujaribu kuokoa uhai wake kwa vile alifikishwa hospitalini hapo akiwa hajitambui.

No comments:
Post a Comment