MWANADADA Ummy Wenceslaus, aliye maarufu kwa jina la Dokii ambaye ni muigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza, ameibuka kujibu tuhuma za baadhi ya watu wanaodai makalio yanayoonekana kwenye filamu yake ya ‘Scandal’ ni ya Kichina.
Akizungumza na Sayari, Dokii alisema watu hao wamekosa la kuongea kwani makalio wanayoyaona ni ya kwake ya kuzaliwa nayo, na kuongeza kuwa anamshukuru mama yake kwa kumzaa na maumbile hayo ambayo yanatatanisha watu hadi kuyaita ya Kichina.
“Nataka waelewe kuwa yale ni maumbile aliyonijalia Mwenyezi Mungu, na wala sina mpango wa kuingia kwa Wachina kumkosoa Muumba,” alisema mwanadada huyo ambaye ni mlokole.
Akiongelea kuhusu sababu ya kuigiza filamu hiyo inayoonyesha bubu akiwa anafanya shughuli za uchangudoa, Dokii anasema ameamua kuja kitofauti, kwani watu wengi amewaona wakipenda kuigiza ulemavu wa kutembea na upofu, huku wakisahau kama kuna wale wasioweza kuongea.
Aidha, alisema ujumbe wake aliokusudia kuufikisha kwa jamii, ni watu kumuogopa Mungu, kwani pamoja na ulemavu aliokuwa nao Surprise wa kwenye ‘Scandal’, lakini watu walikuwa wakimfanyia sivyo ikiwa ni pamoja na marafiki zake.
No comments:
Post a Comment