Sunday, 8 April 2012

ME, I'M STAR FOR NOW AND FOREVER" STEVEN KANUMBA 'THE GREAT' (1984 - 2012)

                              HUU NI MWILI WA MAREHEMU STEVE KANUMBA KABLA HAUJAWEKA KWENYE CHUMA CHA KUIFADHIA MAITI(samahani wadau kwa hii picha)


Hata nikifa leo nitakumbukwa sana..

Marehemu Steven kanumba 'THE GREAT' Superstar wa Bongo Movies aliyasema hayo kwenye Interview aliyofanyiwa na mwandishi wakati alipokuwa Zanzibar Film Festival-ZIFF 2010. 
Kanumba ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo, inasemekana kwamba kifo chake kimesababishwa na ugomvi ulokuwa chumbani mwake Kanumba
kati yake na msanii mwenzake anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'LULU' ambao ulisababisha Lulu kumsukuma naye akaangukia kisogo na hicho ndicho kilichomsababishia umauti.
Lakini hadi tunavyoongea LULU yuko polisi OSTERBAY kwa ajili ya mahojiano na polisi.
Steven Charles Kanumba alizaliwa januari 8, 1984, akiwa ni Msukuma kutoka mkoani Shinyanga alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msingi Bugoyi mkoani humo. 
Alipo maliza elimu yake ya Msingi Kanumba alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Mwadui seminari na baade alipofika kidato cha pili kuhamia katika Shule ya Christian a Seminari iliyopo jijini Dar es Salaam. Alihitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi .
Kanumba amefariki huku akiwa anamfikiria msanii mwenzake Kajala Massanja ambaye yupo Segerea, kwani ndiyo Posti yake ya mwisho alotuma kwenye mtando wa kijamii Facebook. Akilalamika kuhusu roho mbaya walonayo wasanii kwani Kajala yupo Segerea lakini hakuna mtu yeyote katika tasnia ya filamu nchini inayomsapoti msanii huyo. 
Kanumba atakumbukwa kwa mengi sana, Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.
Kanumba alipata mwaliko wa kushiriki katika tamasha kubnwa la Filamu la Nchini Ghana ambalo linajulikana kamam Festival of Films in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.
Taarifa za awali kuhusu kuagwa Mwili wa marehemu zinasema kwamba mwili Steven Kanumba unatarajiwa kuagwa siku ya Jumanne ya tarehe 10 Aprili, pale Leaders Club!

1 comment: