Thursday, 10 May 2012

FAILI YA MASHITAKA YA NASSARI KUPELEKWA KWA DPP!!

FAILI la mashitaka dhidi ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) baada ya upelelezi wa tuhuma zinazomkabili kukamilika. 

Naibu Kamishna wa Polisi nchini Isaya Mngulu, kutoka Idara ya Upelelezi Makao Makuu, alisema hayo jana na kufafanua kuwa DPP ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kufungua mashitaka ama kutofungua dhidi ya Nasari. 

Katika hatua nyingine, Mngulu alikanusha taarifa kwamba Nassari alihojiwa Polisi kwa saa saba na kufafanua kuwa kisheria mtuhumiwa yeyote haruhusiwi kuhojiwa zaidi ya saa 3. 

“Tunaruhusiwa kumhoji mtuhumiwa saa tatu tu, ikizidi mahojiano yanaahirishwa mpaka siku inayofuata na sio kweli Nassari alihojiwa saa saba kwani ni kinyume na sheria,” alisema Mngulu. 

Wakati upelelezi ukiendelea, Mngulu alisema Nassari ametakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha akihitajika atajulishwa kwani kwa sasa bado utaratibu haujakamilika. 

Nassari alikwenda katika kituo hicho majira saa 6.28 akiwa katika gari aina ya Hiace lenye namba 904 ANN akiwa na baadhi ya mawakili wake na wapambe na kwenda moja kwa moja katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Arusha. 
ENDELEA KUSOMA http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29942

No comments:

Post a Comment