Chanzo cha kuaminika cha Ijumaa Wikienda kilichokuwa miongoni mwa mashosti zake waliofika gerezani kumtembelea mwishoni mwa wiki iliyopita (jina kapuni) kilitonya kuwa, wakiwa hapo Kajala alidai akifanikiwa kushinda kesi inayomkabili hatahitaji tena kurudi kwa mumewe huyo ambaye wameshitakiwa pamoja.
“Mwenyewe alieleza kuwa, ndoa ndiyo iliyomfikisha hapo alipo kiasi kwamba anajuta kuolewa, akasema bora apewe talaka yake.
“Tulijaribu kumsihi asiwe na mawazo hayo kwa kuwa kila kinachotokea ni mipango ya Mungu lakini alionekana kushupalia hilo la talaka akidai isingekuwa kuolewa na mwanaume huyo, sasa hivi angekuwa anakula bata mtaani,” alidai mtoa habari huyo.
Kilieleza kuwa, siku hiyo Kajala aliwatoa watu machozi baada ya kueleza kuwa, ndoa yake imemuingiza kwenye matatizo ambayo yamemfanya ashindwe kwenda kushuhudia mazishi ya Kanumba, msanii aliyemfanya asimame kwenye filamu.
Kajala na mumewe wanaendelea kusota kwenye Gereza la Segerea wakikabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu.
No comments:
Post a Comment