Friday, 18 May 2012

KIZIMBANI KWA KUMLAWITI MTOTO WA MWENZAKE!!

MTOTO mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Makunguru jijini Mbeya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume. 

Wakili wa Serikali Emma Msophe mbele ya Hakimu Mkazi Monika Ndyekobolla alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 3 mwaka huu katika maeneo ya Makunguru mkoani hapa. 

Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana . Kesi itatajwa tena Mei 31 mwaka huu. 

Wakati huohuo mkazi wa Maganzo mkoani hapa, Ngao Amosy (55) amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kukutwa akimiliki shamba la bangi . 

Akisomewa shitaka na Wakili wa Serikali Msophe mbele ya Hakimu Ndyekobolla alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Aprili 19 mwaka huu katika maeneo ya Maganzo Halmashauri ya Mbeya Vijijini.
 CHANZO:HABARI LEO

No comments:

Post a Comment