Friday, 11 May 2012

LOWASSA AKATAZA WANACHAMA KUHAMA CCM!!



MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amekuwa akifanya mikutano ya ndani na ya hadhara jimboni humo katika kinachoonekana ni kuzima wimbi lililoibuka hivi karibuni la wanachama wa CCM kuhamia Chadema. 

Tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Mkoa wa Arusha, James ole Millya, limekuwapo wimbi la wana CCM kuhamia Chadema katika mikoa kadhaa nchini. 

Mbali na Millya, wanachama wa CCM wakiwamo viongozi wenye nafasi za udiwani, walitangaza kuhamia Chadema ambayo moja ya ngome zake ni Arusha iliko na wabunge wawili; Arumeru Mashariki na Karatu. 

Chadema pia ilikuwa ikiongoza Jimbo la Arusha Mjini kabla ya matokeo yake kutenguliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM. 

Lowassa alifanya mikutano ya ndani jana eneo la Mto wa Mbu na wa hadhara, ambako aliwaambia wananchi, kwamba pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya yeyote, lakini haoni umuhimu wa wanaCCM kuhama sasa.

No comments:

Post a Comment