Welcome to MaMa J2 blog
News,Entertainment,Beauty,fashion,lifestyle and...Gossip
Pages
Home
Contacts
Advertise With us
Thursday, 17 May 2012
LULU AKWAA GONJWA BAYA!!!
MASKINI Kalulu Kadogo! Habari mbaya zilizotua kwenye dawati la Amani wiki hii zinaeleza kuwa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa gonjwa baya akiwa mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kunaswa kwenye duka linalouza madawa ya binadamu maeneo ya Kinondoni, rafiki wa karibu wa Lulu alidai kuwa alikuwa akinunua dawa za kumpelekea Lulu gerezani kwa kuwa amepatwa na ugonjwa unaomshambulia sehemu nyeti wa
Urinary Tract Infections (U.T.I).
“Namchukulia Lizzy (Lulu) dawa, amepata U.T.I, si unajua mazingira ya usafi kwenye vyoo vya gerezani?
“Ni rahisi sana mtu kupata au kuambukizwa U.T.I kwa sababu ya mazingira ya vyoo vya public (vinavyotumiwa na watu wengi),” alisema rafiki huyo ambaye huwa hakauki gerezani hapo.
Hata hivyo, baada ya kupeleka dawa, Amani lilimpigia simu rafiki huyo ili kujua hali ya Lulu ambapo alidai kuwa anaendelea vizuri huku hofu kubwa ikiwa kwenye ujauzito wake kuhofiwa kuchoropoka.
Lulu yupo nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea kwa msala wa kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’ akitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine Mei 21, mwaka huu.
http://www.globalpublishers.info/
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment