Friday, 11 May 2012

MAMA ADAIWA KUMZIKA MWANAE AKIWA HAI!!!

MKAZI wa kitongoji cha Sokoni Sirari, Mawadawa Joseph (18), anashikiliwa Polisi Kituo cha Sirari, kwa tuhuma za kumzika mwanawe wa kike wa miezi mitatu, Naomi Marko akiwa hai. 

Mawadawa anadaiwa kumfunga mwanawe kwa kamba mikononi na miguuni na kumzika mtoto huyo, baada ya kukataliwa kupewa matunzo na mzazi mwenzake. 

Kamanda wa Polisi Mkoa Maalumu wa Tarime na Rorya, Kamishna Msaidizi, Justus Kamgisha amesema Mawadawa anadaiwa alipata ujauzito na kuzaa na kijana aliyemtaja kwa jina la Marko na baada ya kujifungua, alikosa fedha za matumizi. 

Kamanda Kamugisha alisema Jumanne ya wiki hii majirani wa Mawadawa walipata fununu za kuuawa na kuzikwa mtoto huyo baada ya kutomwona msichana huyo akiwa na mwanawe na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sokoni, Robart Nashon. 
Baada ya taarifa hiyo, inadaiwa Nashon aliungana na wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo na kuanza kumhoji ndipo alipokwenda kuwaonesha alipomzika mtoto huyo. 

Wananchi kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, kwa kushirikiana na polisi walifanikiwa kufukua kaburi alilokuwa amefukiwa mtoto huyo la futi tatu na kukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umefungwa kwa kamba miguuni na mikononi. 

Hali hiyo kwa maelezo ya Kamanda Kamugisha, iliwatia wananchi hasira na kudai kuwa huenda mtoto huyo alizikwa angali hai na kutaka kumshambulia kwa mawe Mawadawa ambaye aliponea chupuchupu baada ya kuokolewa na Polisi Kituo cha Sirari
                                                          chanzo: habari leo

No comments:

Post a Comment