Wednesday, 23 May 2012

MATAJIRI G8 KUMWAGA TRILIONI 1/- TANZANIA!!!

KUNDI la nchi nane tajiri duniani-G8 limeahidi kuipa Tanzania dola milioni 897 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh trilioni 1.3) chini ya mpango maalumu wa kuimarisha kilimo na usalama wa chakula barani Afrika. 

Kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete aliyehudhuria mazungumzo ya wakuu wa nchi hizo uliofanyika katika Ikulu ya Camp David iliyoko Maryland kuhusu kilimo katika Afrika, Ijumaa Rais Barack Obama alitangaza uamuzi huo wa G8. 

Kikwete ambaye alihudhuria mazungumzo hayo, alitangaza jijini hapa juzi alipozungumza na mwandishi wa habari hizi, akisema Marekani ndiyo iliyoahidi kutoa kiasi kikubwa ambacho ni dola milioni 315 (zaidi ya Sh milioni 470). 
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30420

No comments:

Post a Comment