Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, Miriam ambaye alikuwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 480747 iliyotolewa Agosti 17, mwaka jana, alikamatwa uwanjani hapo jana saa 9:00 usiku akiwa tayari kupanda ndege ya Turkish Airline kwenda Uturuki.
Nzowa alisema Miriam alitumia begi kubwa la nguo kwa kuhifadhia bangi hizo zilizokuwa zimefungwa katika mabunda ambayo yako 23, ambapo alitanguliza bangi hizo chini zikiwa zimezungushiwa karatasi ya kaboni ambayo haioneshi kitu kilichomo ndani yake na kisha kuweka nguo juu yake.
“Alikamatwa baada ya mashine ya kukagua mizigo kutoonesha baadhi ya sehemu ya mizigo iliyomo ndani yake, ndipo tukamshuku na tulipokagua ndani, ndio tukakuta dawa hizi, na alikuwa tayari anataka kuelekea nchini Uturuki,” alisema Nzowa.
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30215
No comments:
Post a Comment