Wednesday, 16 May 2012

RC: Katibu Chadema aliyeng’ata sikio ‘ashughulikiwe’

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo ameiagiza Polisi mkoani hapa kuchukua hatua zinazostahili kwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ilemela, Abel Mwesa baada ya kutuhumiwa kumng’ata na kuondoa kipande cha sikio la mkazi wa kitongoji cha Nyabiti. 

Ndikilo ametoa agizo hilo baada ya mlalamikaji, Lazaro Nolbert kufika ofisini kwake na kutoa malalamiko hayo ambayo aliyaripoti katika Kituo cha Polisi Mwatex tangu Aprili 26, mwaka huu, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. 

“Haya ndio mambo yanayolichafua Jeshi la Polisi, mtu ameripoti wiki mbili zilizopita hadi leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa huku akipokea barua za vitisho, jamani hebu chukueni hatua ili jeshi hilo liendelee kuaminiwa na wananchi,” alisema Ndikilo. 
ENDELEA KUSOMA  HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30190

No comments:

Post a Comment