Wednesday, 16 May 2012

SHIBUDA ATANGAZA KUWANIA URAIS AKIWA CHADEMA!!

BAADA ya mwaka 2005 kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kubwagwa katika hatua za awali, Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda, kwa mara nyingine ametangaza kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015. 

Shibuda alitangaza azma yake hiyo juzi mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwenye semina iliyofanyika Dodoma katika ukumbi wa Nec ya CCM iliyojadili hali ya utawala bora nchini iliyotolewa na taasisi inayotathmini utawala bora Afrika (APRM). 

Shibuda ni mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo anayewakilisha vyama vya upinzani. 

"Nakupa pole, kazi ya urais ni ngumu sana, bila shaka utakumbuka kuwa nami nilitaka kuwa mbadala wako, hata hivyo naamini utakuwa meneja wangu wa kampeni za urais mwaka 2015," alisema Shibuda. 
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=30182

No comments:

Post a Comment