Friday, 25 May 2012

ZITTO: KANUMBA ALIOMBA AANDALIWE JIMBO!!!



MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema kwamba marehemu Steven Kanumba alimuomba amuandalie jimbo la kugombea katika uchaguzi mkuu ujao.
Katika mahojiano yanayopatikana kwenye CD ya mazishi ya nguli huyo wa filamu, Zitto alisema marehemu walikuwa wakikutana naye mara kwa mara katika kubadilishana mawazo na kati ya mambo mazito ambayo waliweza kuzungumza ni hilo la kutaka kugombea.
Hata wakati mbunge huyo akiongea maneno hayo,gazeti hili liliwahi kumuuliza suala hilo Kanumba ambaye alikanusha na kudai kwamba haoni haja ya kugombea wakati viongozi wenyewe waliopo madarakani hawajali wasanii wa nchi hii pamoja na kazi kubwa ambayo wamekuwa wanaifanya.

No comments:

Post a Comment