Tuesday, 25 September 2012

MAASKOFU KUWANYIMA WAUMINI SAKRAMENTO!!!

Maaskofu waliopitisha sheria hiyo wamesema kuwa yeyote atakayekosa kulipia kodi ya kanisa ambayo ni asilimia nane ya mapato yao watanyimwa sakramento na kisha kutotambuliwa kama wakatoliki.

Maaskofu hao wameshtushwa na idadi ya watu wanaoendelea kuasi ukatoliki.
Wanasema kuwa hatua kama hii ya kuasi dini itakuwa ni kwenda kinyume kabisa na maadili ya jamii.
Watu wote waliosajiliwa rasmi kama wakatoliki, waprotestandi au wayahudi, hulipa asilimia 8 hadi 9 ya mapato yao ya kila mwaka.
Kodi hiyo ilianza kutozwa karne ya 19 kama fidia ya kutaifishwa kwa mali ya kanisa nchini humo.
Idadi ya wakatoliki nchini Ujerumani ni asilimia 30, lakini idadi ya watu nchini Ujerumani wanaoasi kanisa hilo iliongezeka hadi watu 181,000 mnamo mwaka 2010, huku lawama zikitolewa kwa kashfa nyingi za ngono zilizokumba kanisa hilo wakati huo.
Maaskofu hao wamechukua hatua baada ya kushtushwa na ongezeko la waumini wa kanisa hilo wanaoasi dini, pamoja na profesa mmoja aliyestaafu Hartmut Zapp kutangaza mwaka 2007 kuwa kamwe hatalipa kodi hiyo ingawa atasalia kuwa muumini wa kikatoliki.
Iliarifiwa kuwa profesa huyo alitaka kuendelea kupokea sakramento na kuandelea kutambulika kama mkatoliki ingawa maaskofui walipinga hilo na sasa kesi kati ya profesa huyo na kanisa itafikishwa mahakamani siku ya Jumatano.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment