MKE wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), amehojiwa na Taasisi ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za ufisadi.
Wakati mama huyo, Tina Chenge, akinaswa na kuhojiwa na TAKUKURU kwa rushwa, Chenge mwenyewe ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa ndani na nje ya chama chake kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE-System, alisafishwa na Rais Jakaya Kikwete kwamba hakuna rushwa katika ununuzi wa kifaa hicho.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zilisema kuwa Tina alihojiwa juzi na TAKUKURU na kisha kuachiwa huru wakati uchunguzi dhidi yake ukiendelea.
Haikuweza kujulikana mara moja endapo amehojiwa kuhusiana na vitendo vya rushwa vinavyoendelea kwenye uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo Chenge anawania au la.
Kukamatwa kwa mke wa kigogo huyo na hatimaye kuhojiwa na TAKUKURU, kulithibitishwa jana na Mkurugenzi wa taasisi hiyo nchini, Dk. Edward Hosea.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Hosea alikiri taasisi yake kumhoji mke wa Chenge, lakini hakuwa tayari kusema amehojiwa kwa tuhuma zipi.
“Ni kweli tumemhoji na huu ni mwendelezo wa kuwahoji watu mbalimbali wakiwemo mawaziri, wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa na hakuna atakayebaki bila kuhojiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Dk. Hosea.
Alipoulizwa endapo mke wa Chenge amehojiwa kwa tuhuma za rushwa ndani ya uchaguzi wa CCM, Dk. Hosea alisema mahojiano hayo hayana uhusiano wowote na uchaguzi wa chama hicho tawala.
Hata hivyo, alisema kuhusu suala la rushwa ndani ya CCM, TAKUKURU imeshatoa maelekezo kwa watendaji wake mikoani na ripoti za taarifa hizo zinafanyiwa kazi.
Hivi karibuni, Rais Kikwete alivunja ukimya kwa kuuambia umma kwamba hakuna rushwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini kwa kauli hiyo ni dhahiri kwamba alimsafisha Chenge ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuhusika na kashfa ya ununuzi wa rada kutoka Kampuni ya BAE-System.
Chenge ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anatajwa kuhusika kutoa ushauri wa kisheria wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ushauri ambao unatajwa kuzingatiwa katika hatua za uamuzi.
Mwingine anayehusishwa na kashfa hiyo ni aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Idriss Rashid.
Pamoja na hao, wanatajwa wafanyabiashara wenye asili ya India, lakini ambao wanaishi/walipata kuishi Tanzania, Tanil Somaiya, ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya uwakala wa simu ya Shivacom na Sailesh (Shailesh) Vithlani kuwa watu wa kati wa biashara hiyo.
Akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wahariri aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika na ununuzi wa rada wakati chenji yake imesharejeshwa, Rais Kikwete alisema Serikali ya Uingereza iliyokuwa ikichunguza kashfa hiyo imebaini kuwa hakukuwa na rushwa katika ununuzi bali kulikuwa na makosa ya uchapaji.
Dk. Hosea, alipata mara mbili kunukuliwa akisema Chenge hakuwa na kesi ya kujibu katika kashfa hiyo ya rada.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment