Bwana Cecil huenda akafungwa miaka miwili gerezani ikiwa atapatikana na hatia.
Bunge la Uganda linajadili sheria ambayo italenga kudhibiti maswala yoyote kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.
Mchezo huo, ambao unahadithia maisha ya mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja aliyeuawa na wafanyakazi wake, ulichezwa katika kumbi mbili za michezo ya kuigiza mjini Kampala mwezi jana.
Gazeti moja la nchini humo, Daily Monitor, liliripoti kuwa baraza la kudhibiti habari nchini humo, ilitoa onyo dhidi ya kuuonyesha mchezo huo hadi waandalizi watakapopewa idhini.
Bwana Cecil aliachiliwa kwa dhamana baada ya kulipa dola miambili na kuamrishwa kutoa pasi yake na kisha kurejea mahakamani tarehe kumi na nane mwezi ujao.
Wakili wake John Francis Onyango, aliambia shirika la habari la AFP, kuwa mteja wake yuko bukheri wa afya.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Uganda na watu wameshambuliwa pamoja na kubaguliwa kuhusiana na vitendo hivyo.
chanzo:bbc
No comments:
Post a Comment