KABURI la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba limeanza kujengwa upya ikiwa ni siku chache baada ya wasanii wenzake kushushuliwa kuhusiana na muonekano wake ulivyokuwa.
Hatua ya kulijenga upya kaburi hilo imechukuliwa na Mama yake mzazi, Flora Mtegoa na kampuni ya Steps kutokana na mauzo ya kazi zake mbalimbali za filamu, hivyo wameona ni vyema wakalijenga upya kwani lilikuwa ni gumzo kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihoji hadhi ya kaburi hilo na umaarufu wa marehemu Kanumba.
Akizungumza na paparazi wetu, Mama Kanumba alisema kauli za kaburi hilo kujengwa upya zilikuwa kama wimbo wa taifa lakini kuna mambo alikuwa akiyamalizia, hivyo kwa sasa ameshalijenga vizuri tofauti na lilivyokuwa mwanzo.
“Kaburi la Kanumba tumelijenga upya japokuwa baba yake alisema hakuna haja ya kulijenga tena lakini mimi ndiyo nina uchungu na mwanangu japokuwa ameniacha bado nampenda na nitaendelea kumkumbuka, kwa kushirikiana na kampuni ya Steps tumelijengea vizuri,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni wasanii mbalimbali wa filamu Bongo walilitembelea kaburi hilo na kupatwa na uchungu lakini walishushuliwa na mwenzao na kwa kuwaambia kuwa wamelisusa kaburi hilo.
Alisema hadhi na umaarufu aliokuwa nao Kanumba hakustahili kulala kwenye kaburi lile, hivyo aliwataka kuchangishana fedha ili walijenge vizuri lakini hakuna aliyemuunga mkono badala yake waliishia kupeana maneno mbofumbofu.
Chanzo:http://www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment