Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana imepiga kalenda
kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini, Marijani Abdubakari (50), ‘Papa Msofe’ hadi Januari 22, mwaka huu itakapokuja kutajwa tena.
Hakimu Mkazi Agnes Mchome, alihairisha kesi hiyo baada ya Wakili wa Serikali Ofmedy Mtenga, kuiambia mahakama kuwa upelelezi upande wa Jamhuri haujakamilika.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Papa Msofe anakabiliwa na shitaka la mauaji la Mfanyabiashara mwenzake Onesphory Kitoli, kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Marehemu Kitoli aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa Novemba 6, mwaka juzi, nyumbani kwake Magomeni.
Kabla ya kifo hicho, Papaa Msofe na marehemu walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Sh. milioni 30, kwa makubaliano kwamba marehemu akishindwa kuzilipa hela hizo atachukuwa nyumba yake.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment