Sunday 27 January 2013

Siri vurumai zinazoendelea nchini yafichuka


 Siri ya vurumai zinazoendelea nchini imefichuka kwa kile kinachoelezwa kuwa ni matokeo ya umma kukosa imani na serikali.
Mwanasiasa mkongwe Augustine Mrema , amesema vurumai zinazoendelea nchini ni matokeo ya umma kukosa imani na serikali.
Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam alisema, raia hawana imani na jinsi nchi inavyoendeshwa kutokana na serikali kufanya mambo kiholela kupindukia.
Alisema viongozi na vyombo vya kuhudumia wananchi havitendi haki vinakandamiza wanyonge na kuendesha serikali bila umakini.
Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika awamu ya pili, alisema kuonyesha kuchoka wananchi wanajichukulia sheria mkononi.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment