WAKATI wasanii nchini wakiumiza vichwa vyao kutunga nyimbo ili kujipatia fedha, msanii nyota wa vichekesho Tanzania, Sylvester Mujuni ‘Mpoki’, amesema yeye hutunga kwa ajili ya kufurahisha mashabiki wake.
Akizungumza wakati wa kutambulisha kibao chake kinachokwenda kwa jina la ‘Mademu wa Kibongo’ katika kipindi cha Leo Tena cha Redio Clouds FM juzi, Mpoki alisema kwa sasa yuko katika hatua ya usambazaji wa kibao chake hicho.
Mpoki ambaye anasifika kwa misemo mikali na ya kuchekesha, alisema katika wimbo huo anaeleza sifa za wanawake wanaoishi katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Awali mtayarishaji wa kazi hiyo, Lamar ambaye alikuwa ameambatana naye, aliweka wazi juu ya usumbufu anaopata katika kuandaa nyimbo za Mpoki, akisema kwamba ni mtu wa kuchekesha kila mahala, kiasi kwamba hata waingiapo studio, wakati mwingine hujikuta wakiishia kucheka tu badala ya kufanya kazi.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment