Thursday 11 April 2013

Lady Jaydee kuachia albamu ya sita


MSANII nyota wa kike katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema yuko katika mchakato wa mwisho kukamilisha albamu yake ya sita.
Akizungumza wakati akihojiwa na Magic FM ya jijini Dar es Salaam juzi, Jaydee alisema kuwa katika kuhakikisha albamu yake inafanya vizuri, anawaomba mashabiki kumuunga mkono.
“Nawaomba mashabiki kuniunga mkono katika kufanikisha albamu yangu kufanya vizuri sokoni tofauti na zilizotangulia,” alisema Jaydee.
Alisema albamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni Mei mwaka huu, ikiwa na utofauti mkubwa na zilizotangulia, kwa lengo la kujiongezea mashabiki.
Aliongeza kuwa mchakato wa kuisambaza albamu hiyo ataufanya mwenyewe, kwani alikwisha kuacha kuwatumia wasambazaji wanaotumiwa na wasanii wengine.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment