Wednesday, 15 May 2013

HABARI NJEMA KWA WASANII WA TANZANIA


Waziri wa Viwanda na Biashara ameagiza mabadiliko ya kanuni katika Sheria ya Hakimiliki ili kuhakikisha kwamba wasanii wa muziki hapa nchini wanapata mapato stahiki katika biashara ya “Ring Back Tones” (RBT). Mirahaba katika biashara ya miito ya simu na matangazo ya televisheni na radio. Ni mapato muhimu sana kwa wasanii. Angalau sasa tunaona mwanga. Tutaendelea kuishinikiza serikali kulinda wasanii na hakimiliki zao. Kabwe Z. Zitto, Mb
chanzo:globalpublisher

No comments:

Post a Comment