Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja wa Ndege Nchini, Deusdedit Kato, amesema tukio la Watanzania kukamatwa wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya nchini Afrika Kusini ni baya na limeifedhehesha Tanzania.
Vile vile, amesema tukio hilo limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu hivyo kuna haja ya kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi.
“ Ni lazima tupambane kurudisha heshima kwa sababu watanzania watakuwa hawaaminiki tena katika nchi nyingine, ni mapema mno kuinyoshea kidole taasisi yeyote kwani uchunguzi bado unaendelea ili kubaini aliyeruhusu kupitisha mzigo huo, ”alisema alipoulizwa wasichana hao walikaguliwa.
kukamatwa kwa wasichana hao nchini Afrika Kusini Jumapili iliyopita wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh. bilioni 6.8.
Alisema ni lazima kwa pamoja kufanya uchunguzi na kubaini ni taasisi gani ilipwaya katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuruhusu dawa hizo kupita.
Alisema mpaka sasa uchunguzi umefikia katika hatua nzuri na watatoa taarifa wakati wowote.
Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Polisi,Usalama wa Taifa,Uhamiaji na Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA).
“Tukio hili ni baya limeiitia dosari nchi ambayo ilisifika kuwa na watu waminifu lakini sasa limetuchafua sana, tunahitaji kusaidiana ili kurudisha imani kwa nchi yetu iliyokuwapi hapo awaliaaaa,” alisema na kuongeza:
Wasichana hao inadaiwa kuwa walisafirisha dawa hizo kwa ndege ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.
Taarifa zilionyesha kuwa wasichana hao walikamatwa katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo eneo la Kempton Park Ijumaa iliyopita wakitokea Tanzania.
Wasichana hao walikamatwa na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalikaguliwa na kukutwa na kilo 150 za dawa hizo zinazojulikana pia kama ‘Tik’ zenye thamani ya Randi milioni 42.
Hadi sasa wasichana hao bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa ajili ya upelelezi.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment