MKAZI wa Kijiji cha Muheza, wilayani Chunya, Prisca Msemakweli (30), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Gideon Patson (36) kwa kumkata na shoka kichwani.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Barakael Masaki, alisema jana kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.
Alisema wanandoa hao walianza kugombana baada ya mtuhumiwa huyo kuchelewa kurudi nyumbani akitokea kilabuni.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Masaki kutokana na ugomvi huo, mtuhumiwa alirudi kilabuni na kumchukua hawara wake ambaye hajafahamika jina na kwenda naye nyumbani na kisha kumuua mumewe.
Alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani na kutoa wito kwa watu wenye taarifa juu ya alipo mtuhumiwa mwingine wazitoe katika mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment