Monday, 12 August 2013

Afa akifanya mapenzi gesti

MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi.
Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment