RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.
Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.
Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.
Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.
Kamishna Kova alisema kuwa matukio hayo yamekithiri nchini, ikiwamo tukio la raia wa Lebanon ambaye ni Mkurugenzi wa Home Shopping Centre jijini Dar es Salaam kumwagiwa kemikali iliyomletea madhara makubwa
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment