Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza dau la Sh. milioni 100 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu au mtandao wa wahalifu wa tindikali.
Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova, alitangaza dau hilo jijini Dar es Salaama jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ipo hofu kubwa za watu kujihusisha na uhalifu wa tindikali kimyakimya katika Jiji la Dar es Salaam na wanafanya haraka kubaini mtandao wa watu wanaojihusha na uhalifu huo ili kuudhibiti haraka.
“Tumeona ni hatari sana endapo hatutakomesha haraka mtandao unaojihusisha na uhalifu wa tindikali na ndiyo maana tumeomba tushirikiane na wananchi ili tukomeshe tatizo hili haraka kabla hatujafika pabaya, fedha hizi si za mtu binafsi ni za serikali,” alisema Kova na kuongeza:
‘Hatutaki kuzubaa katika hili, ndiyo maana tumeamua kutoa dau la milioni 100 ili tuwabaini haraka kabla halijatuletea matatizo makubwa kwa sababu ni jambo la kikatili.”
Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yanaokena kushika kasi hapa nchini na huku watu tofauti wakiwa wamefanyiwa vitendo hivyo akiwamo Mhariri Mtendaji wa lililokuwa gazeti la Mwanahalisi, Mkurugennzi wa kampuni ya Home Shopping Centre wa jijini Dar es Salaam, na raia mmoja wa Lebanon.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment