Dar es Salaam. Wakati Rais Jakaya Kikwete akituma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe kutokana na kifo cha Balozi Isack Sepetu, mke wa marehemu amelaumu baadhi ya viongozi wa Serikali, akidai walimtelekeza mumewe kwa kushindwa kushiriki kumuuguza badala yake kuachia familia pekee.
Mariam, ambaye ni mke wa pili wa Balozi Sepetu aliyefunga naye ndoa ya kimila mwaka 1982, alisema mumewe enzi za uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya Ubalozi Urusi na kwamba, kwa kutambua mchango wake, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliagiza agharimiwe matibabu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Akizungumza jana nyumbani kwake, Sinza Dar es Salaam, Mariam alisema alijaribu kuwasiliana na Wizara ya Afya Zanzibar, lakini hakupata ushirikiano aliopata, aliamua kumsafirisha mumewe huyo kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam Oktoba 24, mwaka huu na kumpeleka Hospitali ya TMJ Mikocheni.
“Nishukuru watoto wake wote waliungana na kushiriki kikamilifu kumuuguza baba yao, wakishirikiana na ndugu na jamaa zetu wachache. Kwa kweli jambo hili limenihuzunisha sana nafikiri hakupata huduma ya kutosha,”
chanzo:mwananchi
No comments:
Post a Comment