Wednesday, 30 October 2013

Mugabe aonya mawaziri dhidi ya 'nyumba ndogo'

Mugabe alitoa matamshi hayo wakati wa harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa waaminifu katika ndoa yao, Mugabe alionya dhidi ya kile alichokijata kama tabia ya wanaume kuwa na 'Nyumba ndogo' nchini Zimbabwe akisema kuwa mawaziri wake aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema , pia walikuwa na tabia ya uasherati.
Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe, Mugabe alisema kuwa "mali ambayo baadhi ya waziri wanayo ndio chanzo cha matatizo kwenye ndoa. Nyumba ndogo sio jambo jema na alisema anajua kuwa mawazri wake wote wana tabia ya uasherati ambalo sio jambo jema katika jamii.''
"nawasihi muachane na tabia hiyo . Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka itafanikisha ndoa zenu,'' alisema Mugabe.
Rais huyo wa muda mrefu ametoa changamto kwa wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio kwenye ndoa.
"wanawake lazima wapigane dhidi ya tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo,'' alisema Mugabe.
Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia haupaswi kumaanisha kutupilia mbali tamaduni na maadili.
Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo hualiakwa kwa harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana, huwa hajulishwi.
Alisema tabia hii ndio chanzo cha kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua ugonjwa huo.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment