“Alisema waliwakamata watu 10 ambao wanatuhumiwa kuwa ni wahamiaji haramu kati yao ni wanawake watano na wanaume watano ambao wanawake hao walikuwa wanajihusisha na biashara ya ngono.
“Watu hao wanatoka Tanzania Bara katika mikoa ya Arusha, Kigoma, Mtwara, Mwanza na Songea na walipohojiwa walishindwa kujieleza shughuli wanazozifanya.” Ndivyo gazeti fulani lilivyomnukuu Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mjini kule Zanzibar, Issa Juma Suleiman.
Kama mwandishi alimnukuu vema Kamanda Issa Juma Suleiman, wahenga walikuwa sahihi kuasa: “Heri kujikunguwaa (jikwaa kwenye kitu) guu kuliko kujikunguwaa ulimi.” Ni methali ya kumsema mtu asiyekuwa na hadhari katika usemaji wake, yaani mtu anayesema maneno ovyo.
Kwa hiyo maneno aliyosema mwalimu Oktoba 18, 1961 katika Bunge la Tanganyika jijini Dar es Salaam, yanaoana na methali ya wahenga. Alisema: “Kama uraia wetu utakuwa si jambo la utii wa nchi bali jambo la rangi, hatutaishia hapo … Iko siku tutasema watu wote ni sawa isipokuwa Wagogo, Waha, waliooa zaidi ya mke mmoja, Waislamu n.k.”
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yasema eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Kifungu cha 17 (1) chasema: Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka n-nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
Haki ya raia wa Jamhuri ya Muungano kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano, na kuishi sehemu yoyote, yaani Tanganyika, Unguja na Pemba iko wapi? Kama akitokea kiongozi wa Tanganyika aseme Wazanzibari walioko Tanganyika ni ‘wahamiaji haramu’ ni nani watakaoumia? Muungano utakuwa wa dhati au porojo?
Hivi sasa kuna wafanyabiashara wengi wa Unguja na Pemba wanaoishi Tanganyika katika majumba yao ya fahari na mengine ya kupangisha bila bughudha.
Wametapakaa mikoa yote ya Tanganyika wakifanya biashara masokoni na kumiliki maduka madogo na makubwa, vituo vya mafuta, magari ya mizigo na abiria n.k.
Hawa wakiambiwa wafunganye (funga pamoja vitu au mizigo kwa ajili ya safari), hii iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwapo? Isitoshe Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayomruhusu raia yeyote kuishi na kwenda eneo lolote la Jamhuri ya Muungano itakuwa na maana?
Viongozi wanapaswa kuwa makini sana kwa maneno watoayo kwani maneno ni kama fumo (mkuki) yakitoka mdomoni hayarudi, chambilecho (kama walivyosema) wahenga.

Huu si wakati wa kubaguana kuwa hawa ni Wapemba, wale ni Waunguja na hao ni Watanganyika wakati sote tupo kwenye Jamhuri moja ya Muungano unaoitwa Tanzania.
Arusha, Kigoma, Mtwara, Mwanza na Songea ni baadhi ya mikoa katika Jamhuri ya Muungano kama ilivyo mikoa ya Unguja na Pemba; na kote wamo wafanyabiashara wa Pemba na Unguja wanaoishi bila wasiwasi wakiendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu.

Sasa kusema watu wa mikoa ya Tanzania Bara ni ‘wahamiaji haramu’ inaashiria nini? Ukimya wa viongozi kutokemea kauli hiyo unatia shaka.
Labda nikumbushe tu kuwa Wazanzibari sasa wamegawanyika katika makundi mawili. Moja linataka Muungano uendelee kama ulivyo na jingine lataka Zanzibar iwe huru katika serikali ya Muungano wa mkataba.

Kwamba Zanzibar itambuliwe kimataifa kama nchi huru itakayojiamulia mambo yake yenyewe na kuwa na nafasi yake kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa.
Kwa hiyo kauli kama iliyotolewa na Kamanda wa Polisi kule Zanzibar yaweza kuchochea mvunjiko wa Muungano na kusababisha utengano.

Itokeapo kuwa hivyo, Tanganyika na Zanzibar zitaishi katika hali ya kutoaminiana na kusababisha uhasama kati ya watu waliokuwa katika Muungano mmoja. Itakuwa aibu na fedheha.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment