Thursday, 21 November 2013

Dalali apigwa risasi wakati akiuza nyumba.

Dalali maarufu, mkazi wa Mabibo, Dar, Paulo Charles Bundala anadaiwa kupigwa risasi wakati akiuza nyumba.
Huku akiwa hajui kinachoendelea, ilisemekana kuwa dalali huyo alipigwa risasi na mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Mlindoko.
Habari zilieleza kuwa dalali huyo alikuwa akiuza nyumba ya jamaa huyo yenye namba 610, kitalu 47 iliyopo Kijitonyama, Dar kwa oda ya Benki ya BOA kwa madai kwamba alikuwa na deni kwenye benki hiyo.
Akizungumza kwa masikitiko, Bundala alisema kuwa siku ya tukio alikuwa eneo la Kijitonyama, Dar akitangaza mitaani kwa kutumia gari maalum kuwa nyumba hiyo inauzwa, ikiwa ni baada ya kupewa tenda na kampuni moja ya udalali.
“Tulipofika eneo la tukio, tulisikia milio ya risasi na kabla hatujateremka kwenye gari, nilishangaa kuona natokwa na damu sehemu nyeti na kuishiwa nguvu ndipo wenzangu wakanikimbiza Hospitali ya Mwananyamala,” alisema Bundala.
Bundala alisema kuwa kabla ya matibabu alipelekwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ na kufungua jalada la kesi namba KJN/RB/9229/2013- KUJERUHI.
“Kwa sasa naendelea na matibabu, jamaa alitaka kuondoa kizazi changu ila namshukuru Mungu kuniepusha, sitasahau katika maisha yangu, nikitoka hospitali nitahakikisha nafuatilia kesi kwani nasikia mwenyewe alijisalimisha polisi,” alisema

chanzo:.globalpublishers

No comments:

Post a Comment