Monday, 25 November 2013
Kama ni uzungu wa Kitanzania basi hawa wamepotea njia.
Unaweza kusema kuwa jamaa amepagawishwa na wanawake hawa wawili. Au unaweza ukadhani kuwa mke wa jamaa huyu hayuko naye sana moyoni pengine anaye mwingine huko pembe za chaki anayemridhisha vilivyo na ndiyo maana hata akiona mumewe anahangaika na mdogo wake hajali.
Na ndiyo maana hata pale alipoona mumewe anachukua mpira na kuingia nao chumbani kwa mdogo wake hakujali ingawa baadaye alimwambia kuwa alimuona akiuchukua. Mwanamke gani huyu asiye na wivu? Tena pale alipomruhusu mumewe aingie chumbani kwa mdogo wake eti akamchumu.
Hivi ilikuwa ni lazima hivyo? Au pale mke huyu aliporuhusu eti wote walale kitanda kimoja na mdogo wake lakini wasigusane.
Binafsi naona mke huyo tayari kwa kiwango fulani alishamchoka mumewe na ndiyo maana alikuwa anaachia mambo yaende vile ilivyotokea. Mbona wengine wakihisi tu mahusiano ya mume na shemejie humtimua? Hapa ipo namna.
Lakini pia mume huyo naye bwege kweli kweli. Ataonaje ni sahihi mkewe kumkumbusha amchumu shemeji (mdogo mtu)? Huyo bwana naye ana uzuzu fulani ndani ya kichwa chake. Na pela anapopata mwanya anavurugwa na shemeji bila kushtuka kuwa anaye mke pale pale. Kama ni uzungu wa Kitanzania basi hawa wamepotea njia. Siyo mila na desturi zetu Watanzania.
Kuigaiga huku jamani, kutatuletea balaa. Kwa ujumla inaonekana lipo jambo lililojificha kati ya wanandoa hao. Kama hawajachokana, basi lipo tatizo. Si unajua tena Maisha Ndivyo Yalivyo? Ni yale yale ya kuitana shemeji, shemeji huku anazima taa!
chanzo:nipashe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment