Friday, 28 February 2014

Dogo Aslay: Sijutii matokeo kidato cha nne

BAADA ya kupata matokeo mabaya kidato cha nne, kinda wa muziki wa kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ amesema anatarajia kusoma chuo cha muziki ili kukuza kipaji chake.
Akizungumzia matokeo hayo, Aslay alisema hajasikitika sana kupata matokeo hayo na wala hajakata tamaa ya kuendelea kusoma, kwani anataka kusomea muziki kwa lengo la kuongeza ‘mautundu’ katika kazi zake.
“Nimepata 4 ya pointi 32, kwa sababu nilikuwa nachanganya muziki na masomo, hivyo sijayachukia sana matokeo hayo na kwa kuwa muziki ndio kitu ninachokipenda, nataka kusoma chuo cha muziki na si kupoteza muda kuanza ‘kurisiti’, bado sijajua nitakwenda chuo gani kwa ajili ya masomo hayo,” alisema.

“Wengi wamekuwa wakinisema kwamba napoteza muda mwingi kwa kufanya muziki na kusahau masomo, ndiyo maana nafeli, mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale napenda muziki ndiyo maana nafanya vizuri na ndiyo maana nataka nikaongeze elimu katika muziki wangu,” alisema Aslay.
Dogo Aslay ni kati ya wasanii wenye umri mdogo ambao wanafanya vizuri katika muziki huo, huku akitambulishwa na ngoma yake ambayo ilibamba vilivyo ‘Naenda Kusema kwa Mama’.
chanzo:  tz daima

No comments:

Post a Comment