Wednesday 26 February 2014

Mourinho:jambo la aibu kuona mazungumzo binafsi yanarekodiwa kwa siri.

Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.
Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.
"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.
"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."
Chanzo:bbc 

No comments:

Post a Comment