WAUMINI wa Kiislamu wanaoswali katika Msikiti wa Mji wa Zamani uliopo Mtaa wa Mji Mwema, wilayani Mpanda, wamepigana makonde ndani ya msikiti katika suala la kuamua nani awe imamu wa msikiti huo.
Tukio hilo lilitokea Februari 21, mwaka huu, saa 8 mchana baada ya kumalizika kwa Ibada ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo iliyokuwa ikiongozwa na Sheikh Hussein Mkumba.
Hali ndani ya msikiti huo ilianza kubadilika baada ya swala hiyo ambapo Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Ally Hussein, ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, aliposimama na kuwaeleza waumini hao kuwa hatua inayofuata ni ya kumkabidhi hati ya uimamu mpya wa msikiti huo, Yassin Kasote.
chanzo:tz daima
No comments:
Post a Comment