Tuesday 25 March 2014

Elizabeth Michael ‘Lulu’ kunogesha The Great Foundation

MSANII maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anatarajiwa kunogesha tamasha maalumu la uzinduzi wa taasisi ya Kanumba The Great Foundation, kwenye Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam, Aprili 7.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mratibu wa tamasha hilo, George Wakuganda, alisema kuwa, Lulu amekubali kushiriki tamasha hilo na kila kitu kinakwenda sawa mpaka sasa.
“Lulu amekubali kuungana na wasanii wenzake katika
tamasha hilo kubwa, ambalo litakuwa ni mara ya kwanza
linafanyika tokea kifo cha Kanumba,” alisema Wakuganda na kuongeza kuwa, siku hiyo itakuwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo chake.

Aidha, Wakuganda alisema maandalizi ya tamasha hilo
yanaendelea vizuri kama yalivyopangwa, ambako kabla ya
siku hiyo, kutakuwa na mambo mbalimbali ya kijamii ikiwamo wasanii mbalimbali kutembelea hospitali, magereza, vituo vya watoto yatima na kaburi la marehemu Kanumba.
Aliongeza kuwa baada ya kumaliza zoezi hilo la kijamii, kutakuwa na bonanza maalumu ambalo litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Club, ambalo litashirikisha timu 12 katika michezo mbalimbali.
Alizitaja baadhi ya timu hizo kuwa ni Bandari Veterani,
Multi Choice, Boko Veterani, Bongo Movie, Bongo Fleva,
NMB, Taswa, Tanzania Stars, CXC Africa na NSSF.
Aliongeza kuwa siku ya tamasha kutakuwa na burudani kutoka bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Jahazi Modern Taarab huku upande wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ni Snura, TMK Family, Juma Nature, Afande Sele, Babu Ayoub, Tunda Man, Dogo Janja na Linah.
Wasanii wa filamu ni Wema Sepetu, Patcho Mwamba, Benny
Kinyaiya, Aunt Ezekiel na Dude.
chanzo:tzdaima

No comments:

Post a Comment