Tuesday 4 March 2014

Kijana afungwa pingu,Polisi watoka nduki?

MWANAKIJIJI wa Chalangwa, wilayani Chunya, Mbeya, Medi Wailes, ameshinda na pingu mikononi kwa zaidi ya saa nane baada ya polisi waliomfunga kuwakimbia wananchi waliopinga kukamatwa kwa kijana huyo kwa kosa la kumpinga mwekezaji wa madini.
Kitendo cha kumfunga pingu kijana huyo kilifanyika saa 8 usiku wa kuamkia Machi 2, mwaka huu, baada ya askari polisi kufika kijijini hapo na kuwakamata wananchi wanaompinga mwekezaji, Joseph Mwazyele.

Mwazyele anadaiwa kutaka kufungua mgodi katika kijijiji hicho, jambo ambalo baadhi ya wananchi wanapinga ingawa wanahitaji uwekezaji huo ufanyike.
chanzo:tz daima

No comments:

Post a Comment