Monday 20 June 2011

MBARONI KWA KULAWITI MTOTO WAKE WA KAMBO!!!!!!!!!!!!!

MKAZI wa Kahe Madukani, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Idd Hashimu (25) anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka sita ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kahe.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Yusuph Ilembo, alisema tukio hilo lilitokea Juni 14 majira ya saa 6:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa huyo Kahe Madukani wakati mama wa mtoto huyo alipokuwa shambani.
Alisema siku hiyo mwanaume huyo alimwita mtoto huyo chumbani na kumziba mdomo kisha kumfanyia kitendo hicho.
Alisema kabla mama wa mtoto huyo hajaenda shambani asubuhi aliacha maagizo kwa mtoto huyo na wenzake wawili wafue nguo na aliporudi majira ya saa 12:00 jioni alikuta nguo hazijafuliwa na alipouliza sababu ya kutofuliwa alijibiwa na mtoto huyo kuwa yeye alikuwa chumbani na baba.
Alisema majibu hayo yalimlazimu mama huyo kumchunguza zaidi mtoto wake ndipo mtoto huyo alipomweleza hali halisi na kumfanya mwanamke huyo kutoa taarifa polisi na baadaye mtoto huyo alipelekwa hospitali na kutibiwa kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani.



No comments:

Post a Comment