Thursday 7 July 2011

WASANII WANAPENDA KUANDIKWA MAGAZETINI?

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halijawahi kupelekewa malalamiko yoyote na baadhi ya wasanii kuandikwa vibaya na magazeti mbalimbali hapa nchini, hasa yale ya udaku.
Hayo yalisemwa na Afisa Habari wa baraza hilo bi Agnes kimwaga.
Alisema hawajawahi kupelekewa malalamiko na msanii yoyote kuwa amechafuliwa na gazeti au chombo chochote cha habari, hivyo kwa upande wake anaona kama huenda wasanii hao wanapenda kuandikwa.
Kuhusu taratibu za kuwasidia wasanii mbalimbali hapa nchini, Kimwaga alisema wamekuwa wakikutana nao kila Jumatatu ili kujua changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika kazi zao na kuzipeleka katika ngazi za juu, lengo likiwa katika kuboresha kazi zao, ambapo alidai kadiri siku zinavyozidi kwenda idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka.

No comments:

Post a Comment