MWIGIZAJI maarufu ambaye jina lake lilikuja juu katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amesema kwa sasa hana mpango wa kutoa filamu yake.
mrembo huyo alisema hataki kukurupuka ili naye aonekane tu ametoa filamu, na badala yake anaangalia upepo unavyokwenda katika soko la filamu na kujifunza zaidi.
Hata hivyo alibainisha kuwa utakapofikia wakati wa kufanya hivyo, anataka kutoa filamu ya mfano wa kuigwa na itakayokubalika ndani na nje ya nchi.
“Kwa sasa kwa kweli nitaendelea kushiriki katika filamu za watu pale watakaponihitaji na si vinginevyo,” alisema.
No comments:
Post a Comment