Pages

Wednesday, 5 October 2011

MBOTO: WACHEKESHAJI WENZANGU TUJIUNGE TUTETEE MASLAHI YETU.


MWENYEKITI wa Chama cha Wachekeshaji nchini, Haji Salum ‘Mboto’ amesema kuwa, anasikitishwa na wasanii kushindwa kujiunga na chama hicho hadi sasa.
 Mboto alisema ili chama kiweze kusajiliwa, kinahitaji si chini ya wanachama 15, lakini hadi sasa kina watu wawili tu - yeye na Ujio, hivyo kushindwa kukisajili rasmi.
Kutokana na hali hiyo alisema huenda wachekeshaji wameridhika na vipato wanavyovipata kupitia kazi zao, kwani lengo la kuanzishwa kwa chama hicho, pamoja na mambo mengine, pia ni kutaka kutetea maslahi yao.
Hata hivyo, alidokeza kuwa jambo hilo pia linachangiwa na wachekeshaji wenye majina makubwa ambao awali waliapa kuhakikisha chama hicho hakifiki popote.

No comments:

Post a Comment