Friday, 3 February 2012

WASANII WENGI WAMEJAA ULIMBUKENI WA USUPA STAAAAA!!!!!!!!!

MWIGIZAJI wa siku nyingi Adam Selemani ‘Swebe’, amesema kuwa wasanii wa hapa nyumbani wamejaa ulimbukeni wa u-supa staa, na ndiyo maana wengi hawapendi kushirikiana na wenzao jambo linalorudisha nyuma juhudi za kukuza fani ya uigizaji.
 Swebe alisema hilo ndilo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa wasanii wengi kutoelewana na kuingia kwenye bifu, na hivyo kusababisha tasnia nzima kuonekana kama ya watu wahuni.
Hata hivyo katika hili hakusita kumtaja marehemu Mzee Kipara, kwamba atamkumbuka daima kwa kuwa alikuwa ni mwalimu wake wa nidhamu na ndiyo maana hadi leo anaweza kuishi na wasanii wenzake vizuri.

No comments:

Post a Comment